6/recent/ticker-posts

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia Wafanyakazi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri, akihutubia wakati katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Meo Mosi.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman, akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akitowa salamu za Mkoa wake katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Mwakilishi wa ILO Zanzibar akitowa salamu za Ilo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Mwenyekiti Taifa wa ZATUC, akizungumza na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, kuwahutubia Wafanyakazi katika viwanja vya Amaan.  
Mkurugenzi wa ZANEMA, Dkt. Salaha Salum Salaha, akitowa hutuba ya Waajiri Zanzibar katika sherehe za Mei Mosi  
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi, akimkabidhi Cheti cha Mwajiri Bora Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Bandari Zanzibar Abdalla Juma (kulia) baada ya Shirika lake kuwa ni Mwajiri bora kwa Mwaka huu 2013 sherehe hizo zimefanyika katika Uwanja wa Amaan
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi, akimkabidhi Cheti cha Mwajiri Bora Zanzibar,sekta Binafsi  Mwakilishi wa Hospitali ya Al Rahma, Zanzibar  (kulia) baada ya Hospitali hiyo kuwa ni Mwajiri bora kwa Mwaka huu 2013 sherehe hizo zimefanyika katika Uwanja wa Amaan 
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pamoja na Viongozi wa Serekali na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Mshikamano, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa Zanzibar zimeadhimishwa katika Uwanja wa Amaan.
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Viongozi wa Serekali wakiimba wimbo wa Mshikamano.
Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Mshikamano huku wakiwa wameshikana mojono kuonesha mshikamano.


 Vijana wa Wajasiriamali wakiwa na bango lao lenye ujumbe kama unavyosomeka katika bango lao. 
 Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar wakionesha jinsi wanavyotowa huduma katika Bandari ya Zanzibar wakipita mbele ya mgeni wa heshima.
 Wafanyakazi wa Benk Kuu ya Tanzania wakishiriki katika Mei Mosi.
 Hayo mbabo ya mbwa kachoka ikiburudisha katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani. 
 Maandamano yaliowashirikisha Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali zilioko Zanzibar wakipita mbele ya mgeni wa heshima katika Uwanja vya mpira Amaan.ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Vijana Wajasiriamani wakishiriki katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wagfanyakazi, wakionesha Mshikamano kwa Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali Zanzibar. 
 Wafanyakazi wa Wizara mbalimbali wakishiriki katika maandamano ya kusadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. 
 Vijana wa Scaut wakishiriki katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.  
 Wafanyakazi wa mashirika ya binafsi na Serekali, wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ,akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia huadhimishwa kila mwaka mwezi Mei Mosi.kitaifa imefanyika katika kiwanja cha Amaan. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serekali na Wafanyakazi Bora wa mwaka 2013,baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi Mei Mosi, katika viwanja vya Amaan.

Post a Comment

0 Comments