Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando 'Bungado Day', iliyofanyika leo jijini Mwanza sambamba na uzinduzi wa Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akishuhudia zoezi la upasuaji wa Moyo alipokuwa akifanyiwa mmoja wa wagonjwa wa Moyo ndani ya Hospitali ya Bugando, baada ya kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza leo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo. Picha na OMR
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika wakati wa upasuaji wa Moyo katika Hospitali ya Bugando.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia moja kati ya chupa ya mafuta ya Vaseline, ambayo ni 'Feki' yaliyokamatwa na TFDA, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo sambamba na uzinduzi wa Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo. Picha na OMR






0 Comments