Moja ya barabara ya historia katika mitaa ya ngombuz ni hii ya kisiwandui ambayo ni barabara ya asili ya enzi hizo, barabara hii ilikuwa ikitumika kama barabara kuu katika mitaa ya Unguja inaanzia eneo ambalo hapo mwazo kulikuwa na kituo cha Askari Zimamoto eneo ilikujengwa maegesho ya magari. bara bara hii inazia darajani hadi miembeni kiplefti wakati huo pakiitwa na kuelekea bomani na kidongochekundu,
Kwa ufahamu wangi mimi sijuwi wewe una kumbukumbu gani juu ya barabara hii..Kwasasa inafanyiwa ukarabati mkubwa wa uwekeja wa lami na itatowa huduma na kupunguza msongamano wa magari katika kituo kipya cha daladala.
4 Comments
haya ndo maendeleo tunayoyataka. Hapa kodi zetu zinatumika kisahihi
ReplyDeleteIwe leo basi,Da aminahh!! Baada ya miaka 50 ?? na kwanini ifanyiwe ukarabati iliyopo, jee sizikokuwepo ndani ya mazingira ya mjini kwa miaka 50 tuiteje. Kwahani hakuna barabara,Makadara hakuna ,Chumbuni hakuna ,Msumbiji no road dimbwi mtu,Mpendae hakusemeki,Tomondo usikutaje,sikwambii tena Bububu ndani pakupitwa watu walima mpunga kwa tope.Kiujumla ni serikali iliyofeli kutekeleza wajibu wake.
ReplyDeleteKwa namshukuru allah kwa kuiwezesha serikali yetu tukufu kufikiria na kutekeleza miradi kama hii. Kwa kweli mimi binafsi kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiria saana miradi hii ya ujenzi/uboreshaji wa barabara za ndani ya mji wetu wa Zanzibar. Ni jambo la faraja sana kwani barabaa kama hizi za ndani ya mji mbali na kuweka mandhari nzuru na kupendeza pia husaidia sana kurahisha na kutoa ufanisi katika sekta ya mawasiliano. Lakini kubwa ni pale inapotokea dharura ya kutokupitika kwa barabara kubwa ( kwa mfano wa mafuriko au jambo loolote lile) njia hizi huwa ni mbadala na hivyo kuondoa usumbufu. Pia kutokana na ongezeko la watu na vyombo vya moto kuna haja kubwa ya kutanua mitandao yetu ya barabara ili kuepukana na misongamano mikubwa. Tusome kwa ndugu zetu wa Dar ambapo misongamano ya magari na vyombo vyengine vya moto imekuwa kero kuwa kwa wakaazi wake. Kwa hiyo kuwa miundo mbinu ya barabara za ndani kutasaidia saana kuepusha kero kama hizo.
ReplyDeleteIla wito wangu kuwa tusiishie na barabara hiyo ya Kisiwandui tuu. Kuna maeneo mengi hapa mjini ambapo kuna umuhimu wa kuzifufua na kuziimarisha kwa kiwango cha lami barabara za ndani. Kwa mfano:
(1) Tungeboresha barabara ya ndani itokayo Gulioni shirika la Umeme kuelekea Kwa Abasi HUssein kupitia mitaa ta Shauri moyo, Mboriborini,(kutoka hapo kukawa matawi mawili) moja kuelekea Ziwatuwe kuungana na barabara kuu ya Amani na tawi jengine kuelekea Kwa mtipura kuungana na Barabara ya Benjamin Mkapa (Amaani - Mtoni).
(2) Ili kuondoa msongamani eneo la soko la Mwanakwerekwe, basi tungeikuza na kuiboresha njia ya kutoka Taveta kuelekea Amaani Viwanda vidogovidogo.
(3). Eneo la Kwa boko (Kwa Marhum Kassim Ali), tungeijenga ile njia ya ndani kutokea Viwanja vya Demokrasia kuungana na barabara kuu wa Amani.
(4). Kutoka eneo la Fuoni meli tano msikitini kuelekea Kwarara, tungeikuza hii njia ikaungana ima na njia ya Kisauni kwa upande mmoja na pia ikaungana na njia ya Kwa Mchina auTomondo.
(5)Kutoka kwa Biziredi, Mfereji maringo kupitia baraste kuungana na barabaa ya Mlandege.
(6). Muembe Makumbi kupitiia eneo lililokuwa (mnara wa radio wa zamani) kuungana na barabara ya Benjamini Mkapa.
(7). Kutoka eneo la Soko mboga Mombasa kupitia mitaa ya ndani ya Migombani kungana na barabara ya Jang'ombe school.
Kuna maeneo mengi mengine ambayo imani yangu wadau wengine wanaweza kuyachangia zaidi ambayo yatapelekea kuboresha mji wetu kiwasiliano ya barabara. Najua ni gharama lakini kila jambo linataka azma na nia njema tuu. Kuna mambo mengi serikali huyafanya kwa gharama kubwa sana, lakini ukiyachunguza kwa undani huwa hayana faida sana kwa wananchi wa kawaida.
Ombi langu kwako ndugu yetu Ndugu Othman, kuufikisha hizi comment zetu kwa wahusika tukiamini kwamba kwa nafasi yako utakuwa na ushawishi fulani na sauti ya kusikika mbele ya wakubwa na huenda mawazo yetu yakafikiwa kwa lengo la kundeleza mji/nchi yetu tuipendayo ya Zanzibar. Allah ibariki Zanzibar na watu wake amiin.
Yasikitisha sana kuona katika miaka 50 barabara zilizojengwa ndani ya mji wa zanzibar hazizidi kilomita 15. Mji yetu haijapewa kipa umbele katika miundombinu.. wazee wanaponda mali tu.
ReplyDelete