6/recent/ticker-posts

Balozi Seif Akabidhiwa hati ya Umiliki wa Masjid Muhammad (SAW)

Katibu Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdulla Talib akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa Uamuzi wa Serikali kuruhusu msikiti Muhammad { SAW } uendelea kufanyiwa ibada.Kati kati ni makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na wakwanza kushoto ni Mufti Mkuu wa Zanzibar sheikh Saleh Kabi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikabidhi rasmi hati ya umiliki wa matumizi wa msikiti Muhammad { SAW } kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana  hapo uliopo msikiti huo Mtaa wa Mwanakwerekwe.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mwanakwerekwe kabla ya kukabidhi rasmi hati ya umiliki wa matumizi wa msikiti Muhammad { SAW } kwa waumini hao. 
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu WA Mtaa wa Mwanakwerekwe wakiwa ndani ya Msikiti Muhammad { SAW } wakishuhudia tendo la kukabidhiwa msikiti huo uliokua umefungwa karibu miaka 14 kutokana na hitilafu ya mgongano wa umiliki wa matumizi yake.(Hassan Issa OMPR)

Post a Comment

0 Comments