6/recent/ticker-posts

Mabaki ya jengo la Barafu Sweden


 Ujumbe wa wadi za Makunduchi ulipotembelea mabaki ya nyumba ya Barafu

Utalii wa Kiruna umejengwa kwa nguzo ya ubunifu. Manispaliti inajivunia kwa kivutio cha ICE HOTEL (hoteli ya barafu) ambayo huingiza fedha nyingi sana.
 
Chumba kimoja sio chini ya Euro 4,000 kwa usiku mmoja. Hoteli hii hubeba vyumba zaidi ya 70 na kuifanya kuwa hoteli kubwa duniani ya aina kama hii.
 
Hujengwa karibu na mto ujulikanao Torne River ambao ndio unaotoa mali ghafi ya barafu wakati wa muongo wa baridi. Inasemekana barafu ya Torne River ni ngumu kuliko barafu yoyote ile kutoka kwenye mto.
 
Hoteli hii hujengwa kila mwaka na msimu unapomalizika hubomoka yenyewe kama inavyoonekana wakati tulipoitembelea.
 
Ndani ya hoteli hii hupatikana mapambo mengi yanayovutia ambayo husanifiwa kwenye kuta za barafu. Pengine na sisi tubuni Rain Hotel ili wakati wa masika utalii bado uendelee!

Post a Comment

0 Comments