Ujumbe wa wadi za Makunduchi leo umetembelea kiwanda cha kuchomea taka kwa ajili ya kutoa umeme na kupasha maji moto kwa ajili ya matumizi nyumbani. Taka zinazokusanywa Kiruna huishia hapa. Aidha taka nyengine zinatoka nchini Norway karibu asilimia 45. Norway huilipa Sweden fedha nyingi kwa kusafirisha taka kuzileta hapa. Kutoka kushoto ni Mohamed Muombwa, ndugu Horald, ndugu Abdallah Ali Kombo, bi. Mariam, ndugu Simai Ameir na ndugu Haji Kiongo.
Tangi hili la maji linahifadhi lita 20 milioni. Maji haya huchemshwa kiwandani kwa kutumia taka. Maji haya baadaye husambazwa katika majumba. Wakati wa kipindi cha baridi tangi hili hutumika siku tatu kwani mahitaji huongezeka.Mtaalamu wetu wa maji ndugu Simai Ameir akiuliza swali jinsi maji hayo ya moto yanavyosambazwa majumbani.



0 Comments