Na Mwashamba Juma
Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano, Mhe. Juma Duni Haji, ameahidi kuzifanyia kazi changamoto muhimu
zinazoukabili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.
Alisema uwanja huo umekuwa na
mahitaji makubwa ikilinganishwa na uwezo wake wa kutoa huduma, hivyo unahitaji kuboreshwa
ili kijitosheleza na utoaji wa huduma bora kwa wasafiri
ili hadi yake ilingane na viwanja vyengine vya kimataifa.
Aliyasema hayo jana wakati wa
ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar,kufua uteuzi
mpya uliofanwa na Rais wa Zanzibar hivi
karibuni.
Alisema atashirikiana na
viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pamoja na watendaji wa Wizara yake,
kuishauri serikali kuongeza iadadi ya wawekezaji katika uwanja huoo ili kukidhi
haja ya kuwepo huduma zenye ubora kwa abiria.
“Biashara ni huduma, wasafiri wanahitaji huduma wanazostahili pamoja na
kauli njema ili wafarijike,pia tuwape moyo kwa kuziboresha haraka iwezekanavyo
ili wasivunjike moyo,” alisema.
Alieleza uwanja wa ndege na
bandari ni uso na taswira ya nchi hasa kwa wageni wanaofika kwa mara ya kwanza
nchini.
Alisema haiba njema ya maeneo
hayo zitawavutia wageni kuwa na hamu ya kurejea tena nchini kwa ajili ya
matembezi pamoja na kuitangaza nchi kimataifa.
Akizungumzia usalama kwa
wenyeji na wageni wanaotumia uwanja huo,
alipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa kutekeleza kwa kivitendo sheria za
kimataifa za kutenganisha baina ya wasafiri wa kimataifa na wa ndani ili kupunguza
msongamano.
“Dunia imeharibika kila mmoja
ana hasira zake, hatuwezi kuziba miaya ya watu kwa asilimia mia moja, lakini
kwa kushirikiana tuchukue tahadhari mapema,” alsiema.
Kuhusu tatizo la gari la zima
moto katika viwanja hivyo, alisema
mamlaka inafanyakazi na jumuiya za kimataifa hivyo suala la zima moto ni
muhimu kwa maeneo kama uwanja wa ndege na kuongeza linahitaji ufumbuzi wa
haraka.
Aliwataka wafanyakazi wa wizara
hiyo kumpa ushirikiano katika kutenganeza na kufanikisha malengo ya wiraza kwa
kuhakikisha wanakuwa wakweli na wawazi.
Akitoa ufafanuzi kuhusu maradhi
ya Ebola, Ofisa kutoka mamlaka hiyo, Zaina Ibrahim, alisema mamlaka imejipanga
kukabiliana kwa namna yoyote na ugonjwa huo ili usiingie nchini.
Alisema mamlaka ina utaratibu
wa kukutana na watendaji wa kitengo cha huduma cha uwanja wa ndege ili
kufanikisha mikakati waliojiweke.
“Awali tuliweka mikakati ya
kujikinga wenyewe pamoja na kuwakagua abiria ili kuwatambua wenye maradhi kwa
kutumia kifaa maalum, kusajili wageni wote wanaoingia nchini ili kuwajua sehemu
wanazotoka pamoja na kujua maeneo na muda watakaokaa nchini kwa kueneza fomu
zao wilaya zote na tunawafuatilia muda wote,” alisema.
Alisema hatua nyengine endapo watagundua kama kuna
ndege imeingia nchini na ina mgonjwa wa Ebola, wataitenga mbali na watu ndege hiyo.
Awali akizungumzia changamoto,Mkurugenzi
rasilimali watu wa mamlaka hiyo, Muhidini Talib Abdallah, alisema miongoni mwao
ni kutokukabilika kwa ujenzi wa eneo la abiria wa ndani wakati huduma
zinaendelea, abiria kupata jua na mvua kutoka eneo la maegesho ya ndege hadi
jengoni, msongamano wa wageni wanaoingia na kutoka nchini pamoja na utaratibu
wa kuwahudumia wagonjwa na wanaohitaji msaada.
0 Comments