Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa Nusu Fainal kati ya Muyuni na Makunduchi, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Timu ya Makunduchi imeshinda bao 1--0.
Mshambuliaji wa timu ya Muyuni akimpita beki wa timu ya Makunduchi.
Mchezaji wa timu ya Muyuni akimpita beki wa timu ya Jimbo la Makunduchi, wakati wa mchezo wa Nufu Fainali ya Kombe la Majimbo Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja Amaan.
Viongozi na Wachezaji wa timu ya Jimbo la Makunduchi wakifuatilia mchezo wao wa Nusu Fainal na timu ya Jimbo la Muyuni, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wapenzi wa timu ya Jimbo la Makunduchi wakishangilia bao la ushindi la timu yao, katika mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Benchi la wachezaji wa Muyuni wakipigwa na mshangao baada kufungwa na jirani zao timu ya Jimbo la Makunduchi katika mchezo wa Nusu fainali uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa timu ya Makunduchi wakishangilia bao lililofungwa na mshambuliaji wao Ramso katika dakika za mwisho za mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Majimbo Zanzibar, baada ya kuifunga timu ya Muyuni bao 1--0, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan,
0 Comments