Na Farida Msengwa, Morogoro
WANASIASA wametajwa kuhusika
kwa kiasi kikubwa katika ukatili na mauaji yanayofanywa kwa watu wenye ulemavu
wa ngozi (albino) ili kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na gazeti hili
ofisi kwake,Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Morogoro (TASI), David
Mganga, alisema chama kilifanya uchunguzi na kubaini kwamba mauaji na ukatili
dhidi ya albino yanaongezeka zaidi katika kipindi cha karibu na uchaguzi.
Alisema matukio ya mauaji na
kunyofolewa viungo kwa watu wenye ulemavu, yalishamiri mwaka 2009 na kuanzia
mwaka 2010 lakini yalipungua mwaka 2011.
Aidha alisema yameanza kuibuka
tena mwaka 2014 na kwamba kama hayatadhibitiwa yataendelea kuongezeka hadi
mwishoni mwa mwaka ujao.
Alisema ingawa wanaokamatwa na
viuongo vya albino ni watu wa kawaida
lakini wamebaini kuwa kuna wakubwa nyuma yao ambao wamekuwa wakiagizwa kufanya
ukatili huo.
“Hawa wanaokamatwa ni kumbikumbi
tu, wanaagizwa na viongozi wenye malengo ya kutimiza malengo yao kisiasa ,”
alisema.
Alisema mtu wa kawaida hawezi
kuwa na mahitaji ya viungo vya albino, isipokuwa viongozi wa kisiasa na
matajiri ndio wanaowatuma ili kujinufaisha.
Aliitilia shaka kampeni
iliyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009-2010, kupiga kura ya siri
kuwatambua wauaji wa albino akisema ni ya kisiasa.
Alisema baada ya kampeni hiyo hakukuwa na mrejesho wowote
na kusema huenda mrejesho haukuwa mzuri.
0 Comments