Na Mwantanga Ame
WAKATI mbio za urais wa
Tanzania zikianza, mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM, Balozi Seif Ali
Iddi, amesema Rais mpya anatakiwa awe mtu mwenye sifa wa kuwatumikia Watanzania
na sio mbaguzi wa kidini.
Aliyasema hayo wakati akiwahutubia wanachama wa CCM katika mkutano
wa hadhara uliofanyika kata ya Chiuyu, wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida.
Alisema baadhi ya wanaotaka
urais wanapita kwa wananchi wakiwambia Rais ajae lazima awe Mkiristo wa
madhehebu ya Roman jambo ambalo ni hatari.
Alisema makundi hayo yameanza
kujenga dhana za udini, ukabila na umajimbo, mambo ambayo ni hatari.
Alisema hiyo ni hatari kubwa na
ndio maana Rais wa kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, alikemea ubaguzi na udini.
“Kuna wenzetu wanataka kutuletea ubaguzi,
watuletee nakama, watuletee balaa kwa hivyo tutahadhari na watu wa aina
hiyo,ukija uchaguzi tusizungumze habari ya ukabila wala udini awe Mkiristo au Muislamu,”
alisema.
“Sasa hao wanaotembeza
vikaratasi tuwe na tahadhari nao kwa sababu nchi nyingi zimepata nakama kwa
sababu ya ubaguzi wa ukabila na ubaguzi wa kidini,” alisema.
Alisema atahakikisha anasimamia
kazi kubwa iliyoanzishwa na chama ili kiweze kushika dola katika uchaguzi mkuu
ujao.
0 Comments