Muwezeshaji kutoka TASAF Pemba, Suleiman Ali Said
akizungumza na wananchi walengwa wa shehia ya Ndagoni wilaya ya Chakechake
Pemba, kwenye mkutano maalumu wa kuitambulisha miradi ya kuwapatia ajirza za
muda walengwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa matuta ya kinga maji na barabara
kwa hatua za kifusi
Wananchi walengwa wa shehia ya Junguni Jimbo la Gando wilaya ya Wete kwenye TASAF (III),
wakimsikiliza mtaalamu juu ya namna ya kufanikisha ujenzi wa mtuta ya kinga
maji, kwenye mradi wa kutoa ajira za muda kwao, ambapo mkutano huo uliofanyika
skuli ya Junguni ulikuwa na lengo la kukusanya maoni yao kabla ya kutekeleza
mradi huo
Msimamizi mkaazi wa kiwanda cha kuzalisha mpira Maziwani wilaya ya wete Pemba nd Saleh
Suleiman Massoud kilicho chini ya kampuni ya Agro Tex Ltd, akiwaonyesha maofisa
wa TASAF ambao walisimamisha msafara wao, kuangalia jinsi uzalishaji wa mpira,
wakati maofisa hao wakiwa na ziara ya kuwakagua walengwa kwenye matayarisho ya
miradi ya kutoa ajira za muda shehia za Junguni na Ukunjwi wilaya ya Wete
Pemba,
Mpira ambayo tayari imeshakauka ikisubiri kufungwa pamoja kwa ajili ya kuisafirisha
nje ya nchi kama vile Dubai kwa ajili ya mauzo, ambapo mpira huo unazalishwa eneo
la Maziwani wilaya ya wete kisiwani Pemba na kampuni ya Agro Tax LTD.
Msimamizi mkaazi wa kiwanda cha kuzalisha mpira Maziwani
wilaya ya wete Pemba nd Saleh Suleiman Massoud, akiwaonyesha maofisa wa TASAF
ambao walisimamisha msafara wao kuangalia jinsi uzalishaji wa mpira kutoka
kwenye miti wake, wakati maofisa hao wakiwa na ziara ya kuzikagua kaya kwenye kwenye
matayarisho ya miradi ya kutoa ajira za muda shehia za Junguni na Ukunjwi wilaya
ya Wete.





0 Comments