TANGAZO
Katika kikao cha Baraza la
Wawakilishi kitakachofanyika Tarehe 22/10/2014, Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar linatarajia kupitisha Miswaada miwili ambayo ni; Mswaada wa Sheria ya
Madaili ya Viongozi wa Umma na Kuanzisha Tume ya Maadili ya Viongozi na Mambo
mengine yanayohusiana na hayo.
Serikali imeamua kuwasilisha Mswada
huu ambao utasimamia Maadili ya Viongozi wote hapa Zanzibar waliotajwa kwenye
Jadweli la Mswada huu.
Katika Mswaada huu Kiongozi yeyote wa Umma
aliyetajwa katika Sheria atatakiwa ndani ya kipindi ambacho kimeelezwa katika Mswaada huu kuwasilisha kwa
Mwenyekiti tamko la mali kwa maandishi kuhusu mali zake anazomiliki na
alizonazo wakala wake, madeni anayodaiwa pamoja na mali na madeni ya mwenza
wake, watoto wake au watoto walio chini ya uangalizi wake.
Kwahivyo, Tume ambayo itaanzishwa kwa
mujibu wa Mswaada huu itakuwa na majukumu mengi mbali mbali ikiwemo kupokea na
kuhifadhi tamko la mali ambalo limetolewa na Kiongozi wa Umma chini ya Sheria
hii, Kupokea tuhuma na taarifa za uvunjwaji wa maadili kutoka kwa wananchi,
Kufanya uchunguzi juu ya madai au tuhuma za uvunjwaji wa maadili kwa kiongozi
yeyote wa Umma.
Mswaada mwengine ni Mswada wa Sheria
ya Kufuta Sheria ya Wauguzi na Wakunga (Uanzishwaji wa Baraza la Usajili wa Wauguzi
na Wakunga) Nam. 9 ya mwaka 1986 na kuanzisha badala yake Sheria mpya ya
Wauguzi na Wakunga na mambo yanayohusiana na hayo.
Madhumuni ya kutungwa sheria hii mpya
ni kuleta pendekezo la kufuta Sheria ya Wauguzi na Wakunga, Sheria Namba 9 ya
1986 ambayo imeonekana kwamba imepitwa na wakati na kupendekeza kuanzishwa kwa Sheria
mpya ya Wauguzi na Wakunga ambayo itaweza kusimamia vyema misingiya taaluma na
maadili ya fani hii kuendana na mabadiliko ya nchi kisiasa, kijamii na
kiuchumi. Aidha mswaada huu unakusudia kuanzisha Baraza la na Wakunga
litakalokuwa na wajibu ya kusimamia fani ya wauguzi na wakunga. Miongoni mwa
sababu za msingi zilizopelekea kufuta Sheria hiyo ni Mabadiliko ya Sera ya Afya;
Mabadiliko ya ukuaji wa kiuchumi na kuongezeka mahitaji ya kijamii yanayotokana
na ongezeko la watu na mabadiliko ya kimazingira; Kutanuka kwa taaluma ya
Wauguzi na Wakunga katika taasisi binafsi na za serikali.
Kwahivyo tunakaribisha michango na maoni kwa
wananchi wote katika miswaada hiyo na kwa mtu yeyote anaehitaji nakala ya Mswaada
tunawakaribisha katika Ofisi zetu za Baraza la Wawakilishi zillizopo Chukwani
kwa Unguja na kwa waliopo Pemba tunawakaribisha kwenye Ofisi yetu iliypo
Wete au unaweza kuupata kupitia kwenye
mtandao wetu www.zanzibassemly.go.tz.
Mwisho wa kupokea maoni hayo ni
Tarehe 12 – 10 – 2014.
0 Comments