Na Mwanajuma Mmanga
Jumla ya Mahujaji 391
wanatarajiwa kurudi nyumbani leo wakitokea Makka Saudi Arabia baada kukamilisha
ibada yao ya Hijja.
Wanatarajiwa kusafiri kwa ndege
ya Shirika la Ndege la Oman na kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Zanzibar, saa 11:00 alfajiri.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Ofisa Shughuli za Kiislamu, Ameir Machano Makame,alisema kundi la
pili linatarajia kurudi nyumbani Oktoba
13 ambalo linajumuisha Mahujaji 363 kutoka Jumuiya ya Tawhid, Labaika na Ahlu Sunna.
Kundi la tatu linatarajia
kurudi Oktoba 15 likijumuisha Mahujaji 3802 kutoka Jumuiya ya Ahludawa
wanatarajia kuwasili saa 6:00 mchana kwa ndege ya Oman.
Aidha alisema kundi la mwisho
linatarajiwa kurudi Oktoba 16 likujumuisha Mahujaji 380 kutoka Jumiya
Alharamain.
0 Comments