Na Bakar Mussa, Pemba
Wafanyakazi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Pemba, wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi
wa raslimali watu wa mamlaka hiyo, Rajab Talib Abdalla, wakati akizungumza na wafanyakazi
wa mamlaka hiyo katika hafla ya kuwazawadia wafanyakazi bora.
Alisema katika kipindi kifupi
kijacho mamlaka itaweka vifaa vya usalama katika uwanja huo.
Bado abiria wanaosafiri katika
uwanja huo wamekuwa wakipekuliwa kwa kutumia mikono hali inayosababisha
migogoro baadhi ya wakati.
Alisema miongoni mwa mikakati
ya mamlaka katika kipindi cha miaka
mitano ijayo ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake wanaokaribia kustaafu, ili
wanapomaliza muda wa utumishi wasiwe na hofu juu ya maisha yao.
Nae Meneja wa mamlaka ya uwanja
wa ndege Pemba, Rajab Ali Mussa, alisema kumekuwa na ushirkiano mkubwa katika uwanja
huo kati ya wafanyakazi na mawakala wa mashirika ya ndege jambo ambalo limeongeza
kiwango cha abiria kutoka 250 hadi 300 kwa siku sawa asilimia 11.6.
Alisema ongezeko hilo
limekwenda sambamba na kuwepo ndege 14 kwa siku na mashirika 18 ya ndege
yanayotoa huduma.
Mzee Ali Juma, kutoka Jumuiya
ya Cotwu Pemba, aliwasihi wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuzidisha nidhamu katika
kazi zao za kila siku.
0 Comments