6/recent/ticker-posts

RAIS DK>SHEIN ATOA VIFAA VYA MCHEZO WA RIADHA IKULU


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi vifaa vya Riadha kwa Mwenyekiti wa mchezo huo Wilaya ya Kaskazini B Unguja Juma Hassan Ali wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya Afisa Michezo Wilaya ya Kaskazini A pia mjumbe wa Riadha Taifa  Faida Salim Juma wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Sherry Khamis akionesha baadhi ya Vifaa vya Riadha kwa Viongozi wa Mchezo huo walipofika Ikulu Mjini Unguja kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)kwa mazungumzo na hatimae kuwakabidhi vifaa hivyo alivyovitoa katika kumarisha Mchezo huo hapa Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwapa mawaidha yake mafupi viongozi wa mchezo wa Riadha walipofika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo katika hafla ya kuwakabidhi vifaa alivyoviandaa kwa Mchezo huo katika Wilaya   kumi za Unguja na Pemba katika mpango wake wa kuimarisha na kuupa nguvu mchezo huo,[Picha na Ikulu.]
Viongozi wa Michezo wa Riadha katika Wilaya   kumi za Unguja na Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao leo katika hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya riadha iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Post a Comment

0 Comments