STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 12.2.2015
Akitoa maelezo ya
Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Afya katika kipindi cha Julai hadi
Disemba mwaka 2014, Waziri wa Afya Mhe. Rashid Seif Suleiman aliyasema hayo katika mkutano kati ya uongozi wa Wizara hiyo na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini
Zanzibar.
Alisema kuwa katika kipindi cha miezi sita Julai hadi
Disemba mwaka jana , Wizara ya Afya imetekeleza mambo mbali mbali hasa katika
kuimarisha miundombinu ya afya pamoja na vifaa vya matibabu.
Akitaja miongoni
mwa mambo hayo Waziri Suleiman alisema kuwa n i pamoja na kukamilika na kuanza
kazi za utoaji wa huduma kwa jengo jipya la upasuaji wa maradhi ya ubongo
na uti wa mgongo katika hospitali ya
Mnazi Mmoja.
Jengine ni kuanza
kazi za ujenzi wa wodi ya watoto kwa ufadhili wa Norway, kumaliza ujenzi wa ICU
mpya kupitia ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China katika hospitali
ya Mnazimmoja pamoja na kuanza kwa hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba.
Mafanikio mengine
ni ununuzi wa mashine ya X-Ray katika hospitali ya Mnazimmoja, kuanza kazi za
ujenzi kwa ajili ya utanuzi wa Hospitali ya Micheweni pamoja na ujenzi wa
chumba cha upasuaji, kumalizia wodi ya wazazi na watoto pamoja na chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wete.
Aidha, aliyataja
mafanikio mengineyo ni upatikanaji wa Ambalesi 4 aina ya Landcrucer kutoka
UNFPA ambazo mbili zitatumika Pemba na mbili zitatumika Unguja, kufanikiwa kwa
chanjo ya Rubella kwa asilimia 87 na kupatikana kwa shetria ya Baraza la
Wauguzi na wakunga na mengineyo.
Sambamba na mafanikio
hayo, Waziri Suleiman alieleza changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na ukarabati
wa jengo la kutolea huduma za macho katika hospitali ya Manammoja na ujenzi wa
eneo la kusubiria kwa jamaa za wagonjwa wanaofika katika hospitali ya
Mnazimmoja.
Pamoja na hayo,
Waziri Suleiman alieleza muhtasari wa malengo na mikakati ya Wizara hiyo kwa
mwaka wa fedha unaoendelea ikiwa ni
pamoja na kuimarisha miundommbinu ya faya, huduma za afya kwa jamii ili
kupunguza maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na kuongeza upatikanaji
wa dawa, vifaa tiba na vitendananishi kwa hospitali na vituo vya afya vya
Serikali.
Wizara hiyo pia,
ina lengo la kutayarisha na kupitia miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa
shughuli za afya, kuanzisha mfumo wa kupimia utekelezaji wa wafanyakazi, kuimarisha
mfumo wa ufuatiliaji na tathmini katika sekta hiyo na kuendelea na mchakato wa
kuanzisha vyanzo mbadala vya upatikanaji wa rasilimali fedha ikiwemo Bima ya
Afya.
Kwa upande wake
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alieleza
juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakisha Wizara hiyo
inaendelea kupata mafanikio kwa lengo la kutoa huduma stahiki kwa jamii.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa matayarisho mazuri ya utekelezaji wa
Mpangokazi wake kwa robo mbili kati ya Julai hadi Disemba 2014 huku akisisitiza kuongeza juhudi ili mafanikio
zaidi yaweze kupatikana.
Wakati huo huo, Dk. Shein alifanya mkutano na uongozi wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi ambapo uongozi huo ulieleza majukumu ya Wizara hiyo kwa
kipindi cha miezi sita kuanzia Julai hadi Disemba 2014.
Katika maelezo
yake Dk. Shein alisema kuwa Wizara hiyo inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa
tija inapatikana kwenye sekta ya uvuvi na mifugo huku akisisitiza haja ya
kutumia taaluma, sheria na taratibu katika kutatua mizozo hasa ile ya uvuvi.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa Serikali imo katika kuweka misingi
ya kuhakikisha wavuvi wanavua bahari kuu sambamba na kutafutiwa vifaa
zikiwemo boti za kisasa huku Serikali ikifanya juhudi katika kuimarisha ufugaji
wa samaki kwa lengo la kuinua sekta hiyo.
Sambamba na hayo,
alisema kuwa jitihada za kinga ziendelee ikiwa ni pamoja na kuwapa wananachi
elimu juu ya maradhi yanayotokana na wanyama ili wapate kujikinga.
Mapema Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Abdilah Jihad Hassan, akitoa taarifa ya Utekelezaji Mpangokazi
wa wizara hiyo alisema kuwa miongoni mwa
malengo yaliopangwa kutekelezwa kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuimarisha
huduma za ugani ili ziweze kuwafikia walengwa wote walio katika sekta ya mifugo
na uvuvi.
Aidha, alieleza
malengo mengine kuwa ni kuendelea na ufugaji wa samamki, uvuvi wa kienyeji na
wa kina kirefu, kuongeza uwezo wa watumishi katika nyanja mbali mbali ili
waweze kuwahudumia wananchi kwa urahisi zaidi pamoja na kuimarisha ushirikiano
na taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa kwa lengo la kuendeleza sekta ya
mifugo na uvuvi.
Pamoja na hayo,
Waziri Jihadi alitumia fursa hiyo kwa
niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpongeza Dk. Shein kwa
hatua anazozichukua katika kuiongoza nchi kwa busara na hekima kubwa.
“Tunaamini kwamba
hekima na busara ulizoendelea kuzitoa itakuwa ani chachu katika kuiletea
maendeleo Zanzibar.
Uongozi huo
ulieleza kuwa kutokana na miongozo aliyowapa katika kuendeleza sekta ya Uvuvi
na Mifugo nchini, wavuvi na wafugaji pamoja na wadau wengine katika sekta hizo
wamepata maendeleo makubwa.
Katika mkutano
huo, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, nae alihudhuria.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
0 Comments