6/recent/ticker-posts

Afya Saccos yafanya mkutano mkuu wa mwaka

 Mwenyekiti wa Afya Sacos Othman Mussa Juma akitoa hutuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ushirika huo uliofanyika Ukumbi wa Ecrotanal Mjini Zanzibar. Wajumbe wa Mkutano huo walizimia kuongeza Akiba ya shilingi elfu 30 kutoka elfu 10 kwa mwezi ili kuzidi kujikwamua na Umaskini. 
 Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Madawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Ushirika wa Afya Sacos. Katika Mkutano huo aliwaomba kuzidisha mashirikiano miongoni mwao.
 Baadhi ya Wanachama wa Ushirika wa Afya Sacos wakisikiliza hutuba ya ufunguzi ya mgeni rasmi(hayupo pichani) katika Mkutano wa mwaka wa Ushirika huo.
 Katibu Mkuu wa Ushirika wa Afya Sacos Kassim Issa Kirobo akitoa nasaha zake katika Mkutano huo ambapo aliwaahidi kusimamia vyema Ushirika huo ili utimize lengo la kujikwamua na Umaskini.
 Mmoja wa wanachama wa AFYA SACOS Makame Mussa akichangia katika mkutano huo ambapo aliwasihi Viongozi wake kuwa waadilifu ili Ushirika wao uweze kuwaletea maendeleo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments