Na Maryam Kidko/Salma Nassor- Maelezo Zanzibar.
Viongozi wa Chuo cha Almadrasatul –Lailahailallah iliopo kitope Wilaya ya Kaskazini B imeandaa mashindano ya kuhifadhi qur-ani kwa akina mama watu wazima .
Mashindano hayo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Mpira wa Kombora Kitope Mkarakatini yalijumuisha akinamama kutoka Vyuo vya Wilaya ya Kaskazini A na Kaskazini B pamoja na Mkoa wa Mjini Maghrib.
Mwalimu Mkuu Ustaadh Omar Saidi Moh’d kutoka Almadrasatul- Lailahailallah amesema lengo kuu la madrasa kuandaa mashindao hayo ni kuwashajihisha Wazee kujua umuhimu wa elimu ili na wao waweza kuwasimamia watoto wao kuepukana na vitendo viovu.
Amesema kuwa elimu ya dini ya kiislamu inamgusa kila muislam mkubwa na mdogo hivyo ipo haja kwa waislamu kujitokeza kuitafuta elimu na kusoma Qur-ani kwani ni kitabu kitakatifu kwa waislamu wote.
Mlezi wa Almadrsatul-lailahailallah Khamis Ndende Juma amesema Chuo hicho kimeshashiriki katika mashindanio mbalimbali yakiwemo ya Mkoa na Wilaya na imeweza kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Hata hivyo amewashauri wanaume kujenga tabia ya kuwaruhusu wake zao kushiriki katika madras mbali mbali ili waweze kupata elmu na maadili ya kiislamu,
Akitaja baadhi ya Changamoto zinazoikabili Madrasa hiyo amesema ni ukosefu wa Vyoo pamoja na uhaba wa nafasi ya kusomea Wanafunzi na kuwataka watu wenye uwezo kusaidia ili waweze kupokea wanafunzi wengi zaidi.
Jumla ya Vyuo 9 vimeshiriki katika mashindano hayo yaliyo jumuisha juzuu moja hadi juzuu ya nane.
MWISHO
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBA.
0 Comments