6/recent/ticker-posts

PBZ Yakabidhi Msaada kwa Watoto Yatima na Wazee Kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj

Afisa wa PBZ Ndg Abdalla Jabir akimkabidhi msaada wa Vyakula na Mbuzi Msaidizi Mdhamini wa Makaazi ya Wazee Sebleni Unguja, Bi Tahiya Abdalla kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj kwa wazee hao kuungana na Waislam duniani kusherehekea sikuku hiyo. PBZ imekabidhi kwa Wazee hao mchele mbuzi na Maji.
Msaidizi Mdhamini wa Makaazi ya Wazee Sebleni Unguja Bi Tahiya Abdalla, akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao kwa kuwajali Wazee hasa kipindi hichi cha Sikukuu, na kusema msaada huo umefeka wakati muafaka na kuzitaka Taasisi nyengine kufuata maadili ya PBZ kutoa faida wanayopata katika kazi zao za kibenki kwa kujali Jamii.
Maofisa wa Benki wa Watu wa Zanzibar wakikabidhi sadaka ya Vyakula kwa Watoto Yatima wanaoishi katika Markaz ya Ijtimai Fuoni, ili kusherehekea Sikukuu  ya Eid El Hajj na Watoto wenzao Duniani kuadhimisha kumalizika kwa Ibada ya Hijj ilinayofanyika Nchini Saud Arabia.
Maofisa wa Benki wa Watu wa Zanzibar wakikabidhi sadaka ya Vyakula kwa Watoto Yatima wanaoishi katika Markaz ya Ijtimai Fuoni, ili kusherehekea Sikukuu  ya Eid El Hajj na Watoto wenzao Duniani kuadhimisha kumalizika kwa Ibada ya Hijja inayofanyika Nchini Saudi Arabia.

Afisa wa PBZ Ndg Abdalla Jabir akiwakabidhi msaada wa vyakula na mbuzi Vijana wa Sober house Mombasa Unguja kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya Ibada ya Hijja.  
Afisa wa PBZ Ndg Abdalla Jabir akiwakabidhi msaada wa vyakula na mbuzi Vijana wa Sober house Mombasa Unguja kwa ajili ya kusherejhekea Sikukuu ya Eid El Hajj kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya Ibada ya Hijja. 





Post a Comment

0 Comments