6/recent/ticker-posts

Mkutano wa Kampeni Mgombea wa Urais Dk Shein, Jimbo la Chonga Pemba


Kikundi cha Taarab cha Kanga Gani cha Mzee Profesa Gogo kikitowa burudani wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika kastika viwanja vya mpira Pujini Pemba Jimbo la Chonga. Wilaya ya Chakechake.
Vijana wa CCM wa Jimbo la Chonga wakiingia katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, kwa shangwe kuhamasisha Vijana kumpigia kura Dk Shein. 
Wasanii wa Kikundi cha Wawi Art wakihamasisha Wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpita Pujini Pemba.   
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba wakati akiwasili katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika Jimbo la Chonga Wilaya ya Chakechake Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya mpira Pujini kuendelea na mikutano yake ya Kampeni ya Kugombea Urais wa Zanzibar.uliofanyika katika Jimbo la Chonga Pemba. 


Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chonga alipowasili katika viwanja vya mkutano kuendelea na mikutabno yake ya Kampeni ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi.
Usta. akisoma Quran kabla ya kuaza kwa mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya mpira Pujini Wilaya ya Chakechake Pemba.
Wananchi wa Jimbo la Chonga wakimsikiliza msoma Quran wakati wa mkutano huo wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, viwanja vya Pujini Pemba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg.Modiline Castico, akiwataka Wananchi wa Kisiwan i Pemba kumpa kura ya Ndio Dk Ali Mohamed Shein, kwa maendeleo na kutimiza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya kipindi chake cha Pili cha Uongozi wa Urais wa Zanzibar kuendeleza Amani na Maendeleo ya Wazanzibar
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakifuatilia mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Pujini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Hamdu Shaka Hamdu akiwahamasisha Vijana Kisiwa Pemba kumpigia Kura ya Ndio Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. 



























Post a Comment

0 Comments