MWENYEKITI wa kamati ya Mafaa Kisiwani Pemba, ambaye
pia ni Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akifungua
kikao cha dharura cha kukabiliana na maafa juu ya hali ya Ugonjwa wa
kipindupindu uliojitokeza katika Kisiwa Cha kojani, kikao hicho
kilichohudhuriwa na maafisa wadhamini, wakuu wa Wilaya na makatibu Tawala huko
katika ofisi ya Mkoa wa kusini Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MAKATIBU Tawala kutoka Wilaya mbali mbali kisiwani
Pemba, wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kamati ya Maafa Kisiwani humo,
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, wakati
alipokuwa akifungua kikao hicho kujadili hali ya Ugonjwa wa kipindupindu
uliojitokeza katika kisiwa Cha Kojani.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Mhe:Saleh
Mohammed Jidawi, akitoa taarifa ya hali ya Ugonjwa wa kipindupindu kwa Upande
wa Unguja ulivyojitokeza na jinsi hatua zilivyochukuliwa, wakati wa kikao cha
kamati ya Maafa Pemba ilipokutana.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Dk Mkasha Hija
Mkasha, akitoa taarifa ya hali ya kipindupindu ilivyo katika kisiwa cha Kojani,
wakati kamati ya maafa Pemba ilivyokutana katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa
kusini Pemba, juu ya kutathimi ya ugonjwa huo na mikakati ya kudhibiti
usiendelee kutokea katika maeneo mengine.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MRATIB wa Idara ya Maafa Kisiwani Pemba Khamis Arazak, akitoa taarifa ya uwepo wa vifaa mbali mbali vya kukabiliana na maafa wakati yatakapojitokeza, katika kikao cha kamati ya maafa Pemba ilipokutana.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe:Omar Khamis
Othaman, akizungumza na wajumbe wa kamati ya mafia kisiwani Pemba, ilipokutana
na kuonesha jinsi ya mikakati waliyoichukuwa katika mkoa wake katika kudhibiti
Ugonjwa huo hauenei maeneo mengine.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
0 Comments