Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe (kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti hilo, Dar es Salaam. Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
MASTERCARD YAITAMBUA EXIM BANK TANZANIA KWA TUZO MBILI, IKITHIBITISHA
UONGOZI KATIKA HUDUMA ZA ELITE NA MATUMIZI YA KADI
-
Mastercard leo imefanya ziara yake maalumu katika makao makuu ya Benki ya
Exim Tanzania jijini Dar es Salaam, kuimarisha zaidi ushirikiano wa
kimkakati ka...
7 hours ago
0 Comments