STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
9.12.2015
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na
wananchi pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kote nchini kufanya shughuli za
usafi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dk.
Shein alishirikiana na viongozi mbali mbali wa serikali, wananchi, baadhi ya
watumishi wa Baraza la Mji wa Zanzibar pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara
Maalumu za SMZ na vikosi vya JWTZ kufanya usafi katika soko la samaki Malindi
mjini Unguja.
Akizungumza
mara baada ya shughuli hiyo Dk. Shein aliwakumbusha wananchi haja ya kuimarisha
usafi ambao umekuwa ni utamaduni wa watu wa Zanzibar.
Aliwataka
wananchi kufanya usafi katika maeneo yote ya kazi, makaazi pamoja na maeneo
mengine ili kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na wananchi wenyewe kwa kuwa
hatua hiyo ni kuimarisha afya zao pia.
“Usafi
ndio maisha yetu, ndio afya yetu na ustaarabu wetu hivyo asiyependa usafi
hapendi afya yake” alisema Dk. Shein.
Dk.
Shein alipongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Pombe Magufuli wa kuitumia siku ya maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu kwa kufanya
usafi.
Alifafanua
kuwa uamuzi huo ni wa busara na kitendo cha wengine kufanya usafi na wengine
kuendelea na majukumu mengine maofisini siku ya leo inadhihirisha umakini na
utekelezaji wa kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU”
“Tunaungana
na wenzetu kuandihimisha siku hii ambayo tumezoea kuiadhimisha kwa gwaride
maalum lakini mwaka huu Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Magufuli ametumia busara kuitumia siku hii kuimarisha usafi” Dk. Shein
aliwaambia viongozi na wananchi
walioshiriki usafi pamoja nae.
Mapema
akimkaribisha Mheshimiwa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na
Idara Maalum za SMZ, Mhe Haji Omar Kheri alitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa
kuungana na wanachi pamoja na viongozi katika zoezi hilo la usafi.
Nao
wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipongeza juhudi hizo za viongozi wao
katika kuthamini umuhimu wa usafi katika maeneo yote nchini hasa ikizingatiwa
kuwa kukithiri kwa uchafu ndio kunakosababisha miripuko ya maradhi mbali mbali
yakiwemo maradhi ya kipindupindu.
Hivyo
wananchi hao walitoa pongezi kwa Rais Dk. Magufuli kwa uwamuzi wake huo wa
kuitumia siku ya leo katika kufanya usafi sambamba na kumpongeza Dk. Shein kwa
kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi katika kutekeleza zoezi hilo la
usafi ambapo lina umuhimu mkubwa katika maisha ya mwanaadamu.
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
0 Comments