Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi, kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya CCM, katika hafla iliyofanyika eneo la Tambuka reli, jijini Dodoma, litakapojengwa jengo hilo. Uzinduzi huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi mbalimbali, wakiongozwa na viongozi na wanachama wa CCM, umefanyika leo Jumatano, tarehe 28 Mei 2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanachama wa CCM mara baada ya
kuweka jiwe la msingi ujenzi
wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma tarehe 28 Mei,2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Katibu Mkuu wa
Chama hicho Balozi
Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na viongozi wengine wakisikiliza maelezo
kuhusu hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya CCM JijiniDodoma
tarehe 28 Mei,2025. 












0 Comments