Na.Wizara ya Afya Zanzibar
WIZARA ya Afya Zanzibar imetitilina
saini mkataba wa makubaliano na Taasisi ya Hodari kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya kwenye upande wa kuwajengea uwezo
wafanyakazi.
Akizungumza mara baada ya utiaji
saini makubaliano hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt.Mngereza Mzee Miraji amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imetoa kipaumbele cha kujifunza kwa watumishi wake ili kuendana na
sayansi na Teknolojia.
Amesema Taasisi hiyo itahakikisha
inatoa mafunzo ya mifumo ya kijidijitali ya afya hasa katika kufanya maamuzi ya
haraka kwenye Sekta ya afya ikizingatiwa kuwa ni Taasisi ya mwanzo wazawa mbayo
imekuja kushirikiana katika kufanya kazi katika sekta ya Afya.
Hata hivyo katibu mkuu amesema kuwa wizara ya afya itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kupeleka mbele sekta ya afya na ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa taasisi ya kwanza ya wazawa kutoa mafunzo ya digital health.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu na Mkufunzi
wa Taasisi ya HODARI Dkt.Zeyana Abdallah Hamid amesema kuwa Taasisi hiyo itahakikisha inawajengea
uwezo wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Hospitali katika kuimarisha Mifumo ya Taaria za afya kijidigitali.
Amesema mafunzo hayo watakayoyatoa yatawezesha
kuimarisha matumizi ya taarifa za afya na mifumo, kupitia sera na mipango kazi
ya Afya kurahisisha matumizi utoaji wa taarifa pamoja na kupanga mikakati
kupitia taarifa zinazopatikana kwenye mifumo ya kijidigitali.
Amefahamisha kubwa la kushirikiana na
Sekta ya Afya ni kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta ya
Afya na kuwa na mifumo yenye ubora
Nae Mkuu wa Kitengo cha usimamizi wa Takwimu za Afya kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Abuu Yussuf Ismail amesema Wizara ya Afya inampango mkakati wa kidijitali zinazohusiana taarifa zinazotoka kwenye Hospitali za Wilaya na vituo vya Afya kuzichakata taarifa hizo na kuzifanyia maamuzi mbali mbali juu ya taarifa hizo.
Amesema ushirikiano na Taasisi ya
HODARI utaiwezesha Wizara ya kupata wataalamu
wazuri wa kuzichambua taarifa hizo ili kuzifanyia maamuzi sahihi taarifa hizo
sambamba na kupanga mikakati itakayowezesha utoaji wa huduma kuwa wenye ubora
zaidi.
Mratibu wa mifumo ya Taarifa Wizara ya Afya Zanzibar Fatma Khatib Haji amesema kuwepo kwa Taasisi hiyo kutawawezesha watendaji kupata ujuzi Zaidi na kuondokana na changamoto ya kutozitumia taarifa za afya zinazopatikana kupitia katika sehemu mbali mbali za Wizara hiyo.
Makubaliano baina ya Wizara ya Afya na Taasisi ya Hodari ni ya miaka mitatu ambapo lengo kubwa ni kuwapatia mafunzo yatakayosaidia Serikali kupitia wizara ya afya kuzifatilia taarifa zinazopatikana kwenye mifumo ya kijidigitali ya wizara ya afya.
MWISHO
0 Comments