6/recent/ticker-posts

Mchezo wa Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar 2025/2026, Kati ya Mlandege na Zimamoto Mchezo Uliyofanyika Uwanja wa Mao Zedong Timu Hizo Zimetoka Sare 0-0

Kocha Msaidi wa Timu ya Zimamoto Juma Abdulraham akitowa maelekezo kwa mchezaji wake Mustafa Maneno, wakati wa mchezo wa Lgi Kuu ya PBZ Zanzibar 2025/2026, mchezo uliyofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana 0-0. 

WAKONGWE wa soka visiwani Zanzibar timu ya Mlandege inaendelea kutoa sare katika michezo yake ya ligi kuu ya Zanzibar baada ya juzi kutoka sare tasa na Zimamoto uliochezwa juzi Mao Zedong A. 

Mlandege katika michezo yake minane hii ni sare ya tano ambapo ameshinda michezo miwili na kupoteza mmoja.

Hivyo kutokana na matokeo hayo Mlandege amefikisha pointi 11 na kupaa hadi nafasi ya saba kutoka ya wanane ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KVZ wenye pointi 19.

Kwa upande wa timu ya Zimamoto matokeo hayo imefikisha pointi 15 na kupanda katika.nafasi ya tatu ya msimamo kutoka wa wanne.

Katika mchezo huo miamba hiyo ilionekana kucheza kwa tahadhari na umanikini wa hali ya juu katika muda wote wa mchezo. 

Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 16 leo itaendelea tena Novemba 20 mwaka huu kwa kuchezwa michezo miwili, mmoja  utawakutanisha Mlandege na Malindi Mao Zedong A na mchezo wa kiporo kati ya KMKM na Uhamiaji uwanja wa Mao Zedong B. 

Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Yussuf Idrisa akiwapita mabeki wa Timu ya Mlandege wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya PBZ 2025/2026, mchezi uliyofanyika Uwanja wa Mao Zedong Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.






 

Post a Comment

0 Comments