Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe akizungumza wakati akishiriki uzinduzi wa mpango wa nishati safi
ya kupikia shuleni ambao unalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kutumia
nishati safi ya kupikia, uliofanyika pembezoni
mwa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe amewaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuchangia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia nchini Tanzania ili kuwawezesha wananchi kuacha kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa hivyo kulinda afya na mazingira.
Ametoa wito huo wakati akishiriki uzinduzi wa mpango wa nishati
safi ya kupikia shuleni ambao unalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu
kutumia nishati safi ya kupikia, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa
Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea katika Jiji la
Belem nchini Brazil.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi ya kupikia ameonesha dhamira ya
dhati ya kuwezesha upatikanaji wa nishati hiyo.
Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa akichagiza ‘Agenda 300’
ambayo inalenga kupeleka umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030
hivyo itasaidia wananchi kutumia umeme wa gharama nafuu na kuacha kutumia
nishati isiyo rafiki kwa mazingira.
Prof. Msoffe amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha
nishati hiyo inapatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu ili kumuwezesha kila
Mtanzania kumudu.
Amesema kuwa pamoja na Serikali kutoa maelekezo kwa taasisi
zinazolisha watu zaidi ya 100 kuachana na kuni na mkaa, inaendelea kuchagiza
elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.
Pia, ameeleza kuwa bado wananchi wanahitaji kupata nishati safi
ya kupikia ambapo inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania
wawe wanatumia nishati safi na kuachana na kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia.
Aidha, Prof. Msoffe amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) kwa kuanzisha program
hii kwenye shule na kuwahakikishia Tanzania itaendelea kuwapa ushirikiano ili
kuleta maendeleo endelevu.
Amesema mpango huo si tu unaziwezesha shule kupata nishati safi
ya kupikia bali pia unawajenga wanafunzi kuwa mabalozi wa matumizi ya nishati
safi ya kupikia kwa jamii inayowazunguka.
Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya Nishati kutoka WFP
Tanzania Bw. Geofrey Ndegwa WFP amesema shule ni sehemu muhimu ya kuwekeza
agenda ya nishati safi ya kupikia kwani wanafunzi wanapata ufahamu kuhusu
umuhimu wa matumizi ya nishati hiyo.
Amepongeza juhudi za Serikali za kuhakikisha taasisi zote za
elimu zinaanza kutumia nishati safi ya kupikia kwakuwa zinahudumia idadi kubwa
ya watu (Zaidi ya 100) hivyo kutumia kuni na mkaa kwa wingi na kusababisha miti
kukatwa kwa wingi.
Bw. Ndegwa ametoa wito kwa Serikali kushirikiana na wadau
wakiwemo Shirika la WFP katika kuchagiza agenda ya nishati safi ya kupikia
katika shule zote hatua itakayosaida kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi
yanayotokana na ukataji wa miti.
Nae Profesa Ed Brown kutoka Program ya Moden Energy Cooking
Service amesema kuna fursa kubwa katika kuziwezesha nchi za Afrika ikiwemo
Tanzania kupata nishati safi ya kupikia.
Amesema ni wakati sasa sekta binafsi zikashirikiana na Serikali
katika kuhakikisha agenda ya nishati safi ya kupikia inakua na kusambaa kwa
jamii.
Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe akizungumza wakati akishiriki uzinduzi wa mpango wa nishati safi
ya kupikia shuleni ambao unalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kutumia
nishati safi ya kupikia, uliofanyika pembezoni
mwa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.
Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe akishiriki uzinduzi wa mpango wa nishati safi ya
kupikia shuleni ambao unalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kutumia
nishati safi ya kupikia, uliofanyika pembezoni
mwa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.
Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe (kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wadau walioshiriki uzinduzi wa mpango wa nishati safi ya kupikia shuleni
ambao unalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kutumia nishati safi ya
kupikia, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa
30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea katika Jiji
la Belem nchini Brazil.
Naibu
Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe akiteta
jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Hali ya Hewa na Uchukuzi wa Serikali ya Visiwa
vya Fiji Mhe. Naisa Tuinaceva mara baada ya
uzinduzi wa mpango wa nishati safi ya kupikia shuleni ambao unalenga
kuziwezesha taasisi hizo za elimu kutumia nishati safi ya kupikia, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.
0 Comments