Na.Wizara Afya Zanzibar.
TAASISI ya The Same Quality Foundation iliopo Arusha Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana Hospitali
ya Lumumba inaendelea na kambi ya upasuaji midomo wazi kwa watu wenye matatizo
hayo ikiwa ni muendelezo wa kambi zinazofanywa na taasisi hiyo ili kuhakikisha
watoto wenye tatizo la midomo wazi wanapatiwa matibabu.
Akizungumza katika kambi ya matibabu
hayo, Dkt Samuel Seseja amesema katika
kufanikisha hatua ya kuwapatia matibabu kwa watu ambao wanatatizo hilo amesema watakuwepo
katika Hospitali hio kwa muda wa wiki mmoja kwa lengo la kufanya upasuaji
wakiwa na wataalamu wao
kushirikiana na baadhi ya
wataalamu wa hapa nchini.
Dkt Samuel ameisisitiza jamii ambao wanatatizo
la midomo wazi kufika haraka hospitali ya Lumumba kwa lengo la kuwapatia matibabu
na yanatolewa bila malipo yoyote ili kuimarisha
zao na kusaidia jamii kuondokana na tatizo hilo.
Ameishukuru Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa mashirikiano makubwa walioyaonesha kwani wamefanya kazi hio kwa miaka kumi na moja katika Hospitali za Unguja na Pemba ikiwemo Abdalla Mzee Mkoani na Mnazimmoja.
Mzazi wa mtoto aliyefika Hospitalini hapo kwa
ajili ya kupatiwa matibabu ya mwanawe Mariyam
Ali Omar amesema mtoto wake anaendelea vizuri na kwa sasa anaweza
kuzungumza na kutamka maneno vizuri na amewasisitiza wazazi ambao wana watoto
wenye tatizo hilo kuwafikisha hospitalini wataalamu watawahudumia bila shida
yoyote.
Wananchi waliofika kupatiwa huduma na Taasisi hiyo wamesema wamepata matibabu mazuri na kuwataka waendelee kutoa misaada ya kiafya kwa huduma kwa wazanzibari na Tanzania kwa ujumla ili kuwa na taifa imara.
Taasisi ya the same Quality Foundation inafanya kazi kubwa ya kusaidia jamii kwa kutoa huduma mbali mbali za Afya Tanzania Bara na Zanzibar hasa kuwapatia huduma watoto na watu wazima wenye matatizo ya midomo wazi na wapo hapa Zanzibar kwa muda wa wiki moja kutoa huduma hiyo.
0 Comments