6/recent/ticker-posts

Michuano ya NMB Mapinduzi Cup Zanzibar Kati ya URA na Mlandege Mchezo Uliyofanyika Uwanja wa New Amaan Complex.Timu ya URA.FC Imeshinda Mchezo Huo Kwa Bao 1-0

 

MSHAMBULIAJI wa Timu ya URA FC  ya Uganda Tusuubira Abraham akimpita beki wa Timu ya Mlandege Vellim Nashon, katika mchezo wa kombe la NMB Mapinduzi Cup 2026, mchezo uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar. Timu ya URA FC. imeshinda mchezo huo kwa bao 1-0.


NA MWAJUMA JUMA 

MATUMAINI ya timu ya Mlandege ya kuendelea kutetea taji lake la Mapinduzi yamezidi kufifia baada ya kufungwa na URA FC bao 1-0, katika mchezo uliochezwa  uwanja wa New Amaan Complex. 

Mlandege kipigo hicho ni cha pili mfululizo ambapo mchezo wake wa kwanza ilifungwa kwa idadi ya magoli 3-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo inayoshirikisha timu 10 kutoka visiwani Zanzibar,  Tanzania Uganda.

URA FC walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa mchezaji wake Amaku Fred lililotolana na uzembe wa.mlinda.mlangp ambae alitoka nje ya lango lake kufuatia kuokoa shambulizi la mbali, huku walinzi.wake.walishindwa kukava kosa.hilo na mpira huo kuingia moja kwa moja wavuni kutokea upande wa kona ya lango la kaskazini.

Kuingia kwa bao hilo kulizidisha kasi ya mashambulizi yaliyonogesha mashabiki kiasi ambao waliingia uwanjani hapo kufuatilia pambano hilo.

Hata hivyo licha ya mashambulizi hayo lakini wanaune hao walidiriki kwenda mapumziko wakiwa URA wakiongoza kwa bao 1-0. 

Kipondi cha pili kilianza na mashambulizi yakaendelea kama kwaida huku kila uapnde wakijaribu kufanya mabadiliko ili kujiimarisha katika safu zake.

Mlandege walifanya mabadiliko kwa kuwapumzisha Abdalla Salum Sio na Alex Gidion Chidou na Suleiman Juma Kidawa na nafasi zao kuchukuliwa na Yussuf Suleiman Haji "Jusa" , Laurent Matius na Ibrahim Samuel.

Kwa upande wa timu ya URA ambao wao ni nchezo wao wa kwanza waliwapumzisha Namanya Norman na mfungaji wa goli Amaku Fred na kuwaingiza  Kabonge Nicholas na Senkatuuka Nelson.

Hata hivyo licha ya kufanyika kwa manadiliko hayo hakukuweza kubadilisha ubao wa matokeo na kumalizika kwa mchezo huo kwa URA FC kushinda kwa ushindi huo mwembamba wa goli 1-0.

Katika mchezo huo mchezaji bora wa mechi ni Masemba George kutoka timu ya URA FC na mchezaji mwenye mchezo.wa kiungwana alitokea timu ya Mlandege ambae ni Jamal Saleh Ali "Jaku".

Mlandege inatarajiwa kushuka dimbani tena Januari 2, mwaka huu, kukutana na Azam FC, ambao utapigwa majira ya saa 2:15 za usiku, mchezo ambao kwa Mlandege utakuwa ni wa kukamilisha ratiba.













Post a Comment

0 Comments