Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini
Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Isaac Njenga Ikulu Jijini Dar es Salaam
tarehe 17 Desemba 2025. Balozi wa Kenya Mhe. Isaac Njenga alifika Ikulu Jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga Mhe. Rais Dkt. Samia ambapo pamoja na mambo
mengine walizungumzia kuimarika kwa uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji baina
ya Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Kenya nchini
Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Isaac Njenga Ikulu Jijini Dar es Salaam
tarehe 17 Desemba 2025.

0 Comments