Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16 Januari 2026.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha Sekta ya Uchukuzi inaimarika ili
kuliweka Taifa kwenye nafasi nzuri ya ushindani wa kibiashara, kuongeza mapato
ya fedha za kigeni na kukuza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Amesema pamoja na ujenzi wa jengo hilo, Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kikamilifu kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kisekta kama ilivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050, Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa na Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2025).
Makamu wa Rais amesisitiza kwamba, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali katika Viwanja vya Ndege, huduma za usafiri wa barabara, usafiri majini na usafiri kwa njia ya reli. Halikadhalika amesema, Serikali itaendelea na uboreshaji wa huduma za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa lengo kuboresha usafiri wa ndani, kuunganisha Tanzania na nchi nyingine, kupunguza gharama za usafirishaji na kuimarisha uchumi wa Tanzania na biashara za kimataifa.
Vilevile, Makamu wa Rais amesema ili kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji, Serikali imedhamiria kuunganisha huduma za Sekta ya Uchukuzi, kama vile uunganishaji wa huduma za Viwanja vya Ndege, usafiri wa barabara, maji na reli. Mathalan, mradi wa kimkakati unaoendelea wa ujenzi wa barabara za Mwendokasi (BRT) kati ya eneo la Posta na Gongo la Mboto utaunganishwa na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ili kurahisisha huduma za usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
Hali kadhalika, hatua za utekelezaji zinaendelea ili kuhakikisha huduma za reli zinaunganishwa na viwanja vya Ndege vya kimataifa, hususan Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro.
Aidha, Makamu wa Rais amesema Jitihada hizo kubwa zinazofanywa na Serikali zinalenga kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi kitaifa na kikanda. Ameongeza kwamba, hiyo inatokana na fursa na faida za kijiografia za Tanzania, ambayo ni lango kuu la biashara la nchi zaidi ya nane zilizopo Kusini, Mashariki na Kati ya Bara la Afrika, na kiunganishi cha Bara la Afrika na nchi za Mashariki ya Kati na Mbali.
Makamu wa Rais amesema, dhamira ya Serikali ni kuendeleza utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo, ujenzi wa reli ya kisasa kwa vipande na maeneo yote yaliyobaki
kuelekea Tabora, Mwanza na Kigoma hadi Musongati (Burundi), uboreshwaji wa
Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine za kimkakati za Tanga, Mtwara,
Kisiwa Mgao, Mbamba Bay, Kigoma na Bagamoyo, uboreshaji wa reli ya TAZARA,
ujenzi na ukarabati wa barabara za lami zinazounganisha Tanzania na nchi za
jirani.
Pia, Makamu wa Rais amesema uwekezaji
wa Serikali katika Sekta ya Uchukuzi umeleta manufaa makubwa. Mathalan,
mchango wa Sekta ya Uchukuzi katika Pato
la Taifa uliongezeka kutoka 7.2% (2023) hadi 7.5% (2024). Kasi ya ukuaji wa
Sekta ya Uchukuzi iliongezeka kutoka 4.1% (2023) hadi 4.2% (2024) na katika
kipindi cha hivi karibuni ilikua kwa
wastani wa 5.4%.
Makamu wa Rais ametoa
rai kwa kwa Watanzania wote kutambua wajibu wa kuilinda na kuitunza miundombinu
inayoendelea kuwekezwa na Serikali kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake Waziri
wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Wizara itaendelea kuhakikisha miradi
ya Viwanja vya Ndege nchini inaendelea kutekelezwa ili kuongeza huduma ya
usafiri wa Anga na hivyo kufungua na kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi
nchini.
Amesema Serikali katika
kuhakikisha inaendelea kuimarisha shughuli utalii, biashara na kilimo,Wizara
kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania inaendelea na hatua za upembuzi
yakinifu na usanifu wa kina ya viwanja vipya vya Serengeti, Kagera na Njombe na
mara baada ya kukamilika itatafuta fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi
hiyo.
Awali akitoa taarifa ya
mradi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege, Abdul Mombokaleo amesema mradi huo ni sehemu ya utakelezaji wa mpango
mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kuhusu uimarishaji wa
Miundombinu na huduma za Viwanja vya Ndege.
Jengo la Viongozi
Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam, limejengwa mahsusi kwaajili ya kuhudumia wageni na Viongozi mashuhuri
wa ndani na nje ya nchi. Jengo hilo ni hatua muhimu katika kuimarisha taswira
ya Taifa na kuongeza hadhi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
katika ngazi ya kimataifa.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akikata utepe kuashiri uzinduzi rasmi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe
16 Januari 2026.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akimkabidhi Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, mfano wa funguo ya
Jengo la Viongozi Mashuhuri, wakati wa uzinduzi wa jengo hilo katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16
Januari 2026.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16
Januari 2026.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akitembelea Jengo la Viongozi Mashuhuri mara baada ya kuzindua jengo hilo
katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam, leo tarehe 16 Januari 2026.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16
Januari 2026.
Viongozi,
Mabalozi pamoja na Wananchi mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati wa
uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16 Januari 2026.
Viongozi,
Mabalozi pamoja na Wananchi mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati wa
uzinduzi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 16 Januari 2026..jpg)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa
na Viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi na
Wawakilishi wa Mashirika Kimataifa walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Jengo la
Viongozi Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam, leo tarehe 16 Januari 2026.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais 16 Januari 2026 Dar es Salaam.
.jpg)




.jpg)


0 Comments