6/recent/ticker-posts

Mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Umeme Yawasili Zanzibar

Awamu ya kwanza ya mradi wa Mabasi yanayotumia Umeme (Zan Bus) imewasili kupitia Bandari ya Malindi, Zanzibar, na kuelekea katika maegesho ya Stendi Mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mabasi hayo 10 yaliyowasili jana alasiri tarehe 25 Januari 2026 yanatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria mwezi Februari, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki wa mazingira Zanzibar.

Aidha, Mradi huo, unaotarajiwa kuendelea kutekelezwa hatua kwa hatua, unaratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini.

Mradi wa mabasi ya umeme (Zan Bus) ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.



 

Post a Comment

0 Comments