Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na viongozi mbali mbali, waendesha Bodaboda na Bajaji na wananchi waliohudhuria katika Tamasha la Samia Bodaboda na Bajaji Festival linalofanyika katika viwanja vya Maisara Complex Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR )Tarehe 26.01.2026.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo mstari wa mbele katika kuziwezesha Taasisi zisizo za kiserekali kwa kuhakikisha zinafanya kazi kwa uweledi na kufikia malengo waliyojiwekea.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika Tamasha la Samia Bodaboda na Bajaji Festival linaloakisi kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalofanyika katika Viwanja vya Maisara Complex Zanzibar.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi zisizo za kiserikali na itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na taasisi hizo kwa lengo la kuleta maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa Tamasha la Samia Bodaboda na Bajaji linafanyika kwa lengo la kutambua mchango wa vijana wa Bodaboda na Bajaji katika kukuza uchumi, ajira na usafiri kwa wananchi.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais amesema amefarijika sana kuona Tamasha hilo limejumuisha utowaji wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha Bodaboda na Bajaji hatua mbayo itapunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka madereva Bajaji na Bodaboda kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za usalama barabarani, kuacha kuendesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali na vifo zisivyokuwa za lazima.
Hata hivyo Makamu wa pili wa Rais amewaelekeza madereva wa bajaji na Bodaboda kuweka utaratibu wa kuwatambua madereva wao ambao utawasaidia kupatikana kwa haraka taarifa zao pindi kutakapotokezea changamoto ya aina yoyote
Amewataka madereva wa Bodaboda, Bajaji na wananchi kwa ujumla kuwa mabalozi wazuri wa kusambaza elimu iliyotolewa katika Tamasha hilo ili kuweza kuwafikia wananchi wengi na kupatikana kwa nabadiliko chanya hasa katika masuala ya usalama barabarani.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema wizara ya afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation ( MIF ) wameweza kuhakikisha katika Tamasha la Samia Bodaboda na Bajaji zoezi la upimaji wa afya na uchangiaji wa damu salama linakwenda vizuri kama lilivyopangwa na wananchi wanapata huduma hizo pasipo usumbufu wowote.
Dkt. Mngereza amefahamisha kuwa katika Tamasha hilo kitengo cha damu salama kinatarajia kukusanya zaidi ya Unit elf mbili (2000) ambapo ametowa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu ambayo itakwenda kusaidia katika kuokoa maisha ya wtu wenye uhitaji ya kuchangiwa damu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) Bi.Sabra Ali Mohammed amesema lengo la kufanyika Tamasha la kuadhimisha siku ya kuzaliwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kurudisha shukurani kwa jamii na kufikisha ujumbe kwa vitendo kwa kuandaa shughuli mbali mbali zinazoigusa jamii moja kwa moja.
Amesema kupitia Tamasha hilo wananchi watapimwa afya bure, kuchangia damu salama pamoja na kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa kuchangia damua pamoja na kuepukana na maradhi yasiyo ya kuambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa nchini.
Sabra amesema ili kuwa na Taifa lenye kupiga hatu kimaendeleo lazima kuwepo na watu wenye Afya Imara hivyo Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation itahakikisha inaendelea kutoa ushirikiano na kuekeza katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya .
Mwenyekiti wa shirikisho la Bajaji na Bodaboda Zanzibar ndugu Abdalla Abdalla amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuona umuhimu wa kurasimisha usafiri wa Bodaboda na Bajaji na kuwa usafiri rasmi unaotambulika katika utoaji wa huduma ya usafiri nchini.
Amesema shirikisho la Bajaji na Bodaboda limekuwa likikabiliwa na chamgamoto mbali mbali ikiwemo tozo na adhabu kubwa zinazotolewa na mamlaka husika jambo linalokwamisha utendaji kazi wa shirikisho hilo lakini pia baadhi wa watendaji wa mamlaka zinazosimamia masuala ya usafiri na usimamizi wa mji mkongwe wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa madereva wa bajaji na Bodaboda.
Katika tamasha hilo makamu wa pili wa rais wa Zanzibar alipokea maandamano ya waendesha boda boda na bajaji sambamba na kukagua mabanda ya wachangiaji damu ambapo ndio lengo kuu la tamasha hilo..jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments