Naibu
Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi
akizugumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Mpango kazi wa Kitaifa
na hatua za utekelezaji wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji kinachofanyika
mjini Morogoro leo Januari 26, 2026.
Serikali kupitia
Ofisi ya Makamu wa Rais imezindua Kikosi cha Kuandaa Mpango kazi wa Kitaifa na
hatua za utekelezaji wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji (MSP) ili
kuimarisha Uchumi wa Buluu.
Kikosi hicho
kimezinduliwa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Abdallah Hassan Mitawi kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.
Richard Muyungi mjini Morogoro leo Januari, 2026.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Kikosi, Bw. Mitawi amesema Mpango kazi wa Kitaifa wa
Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji ni nyenzo muhimu inayotegemewa katika
kuwezesha utekelezaji wa masuala ya Uchumi wa Buluu kwa kuzingatia uhifadhi wa
mazingira na ustawi wa jamii.
Alisema kuwa
uandaaji wa mpango unaoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Shirika la The
Nature Conservative (TNC) na kazi huo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha Serikali
inafanikiwa kupanga matumizi endelevu ya maeneo ya maji.
Bw. Mitawi
alisema Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (2024) na Mkakati wake wa utekelezaji
(2024 - 2034) inasisitiza kupanga matumizi ya rasilimali za maji kwa njia
jumuishi na endelevu, hivyo kufanikiwa kuandaliwa kwa mpango kazi huo utasaidia
katika kutekeleza majukumu ya kila kamati
inayohusika kuandaa MSP kitaifa.
“Mpango kazi ni
lazima kuhakikisha uratibu madhubuti wa kitaifa kuheshimu kila upande unaotumia
bahari, unahitajika msikamano wa kitaasisi kuhakikisha manufaa ya bahari yanawafikia
wananchi wote hivyo, MSP ni chombo cha kuimarisha rasilimali zetu za bahari na
ukanda wa pwani,” alisema.
Aidha, Bw.
Mitawi alisema uvuvi, usafirishaji kupitia bahari, utalii, nishati, utafiti wa
kisayansi na uhifadhi wa bayoanuayi bila upangaji makini shughuli hizi zinaweza
kuleta mgongano wa matumizi ikiwemo uharibifu wa mifumo ikolojia na upotevu wa fursa za kiuchumi hivyo, mpango
kazi huo utakuwa ni chombo muhimu cha kusaidia kukabiliana na changamoto hizo.
Pamoja na hayo Naibu
Katibu Mkuu amesema Serikali inatambua na kushukuru Shirika la TNC kwa kuwa
wadau muhimu katika kuandaa mpango kazi huo wa matumzi ya rasilimali za maji
kwa maendeleo endelevu.
Kwa upande waka
Kaimu Meneja wa Usimamizi wa masuala ya Bahari Bw. Emmanuel Mpina kutoka TNC alisema
wataendelea kushirikiana na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo
ndiyo msimamizi mkuu wa mazingira kuhakikisha kuwa sekta ya uchumi wa buluu
inaendelea kuimarika
Alisema mchakato
wa uandaaji wa mpango kazi huo ulianza tangu mwaka 2019 ambapo uliambatana na kufanya
tathmini ya awali na namna nchi inaweza kuandaa MSP.
Hivyo, Bw. Mpina
alisema matumizi ya vyanzo vya maji yakiwemo usafirishaji, utalii na uvuvi yakifanyika
bila mpangilio yanaweza kusababisha kukosekana kwa fursa za maji na manufaa kwa
wananchi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Finahappy Kimambo alisema mwananchi wa kawaida anaweza kunufaika na mpango kazi huo kwa kupitia shughuli anazofanya zikiwemo uvuvi na kilimo cha mwani.
Aliongeza kuwa Serikali imeamua kuandaa mpango kazi wa matumizi endelevu ya maji kwasababu kwenye bahari kama ilivyo nchi kavu kuna shughuli na wadau wakiwemo wavuvi, wasafirishaji, wachimbaji wa madini na mafuta hivyo, ili kuwa na matumizi endelevu lazima kuwe na mpango wa matumizi.
Kikosi kazi cha kuandaa Mpango kazi wa Matumizi Endelevu ya Maji na utekelezaji wake kinaundwa na wataalamu kutoka Wizara za kisekta, taasisi za serikali na wadau wa maendeleo.
Kaimu Meneja wa Usimamizi wa masuala ya Bahari kutoka
Shirika la The Nature Conservative (TNC) Bw. Emmanuel Mpina akizungumza wakati
wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Mpango kazi wa Kitaifa na hatua za
utekelezaji wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji kinachofanyika mjini
Morogoro leo Januari 26, 2026.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.
Fainahappy Kimambo akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Kikao cha
Maandalizi ya Mpango kazi wa Kitaifa na hatua za utekelezaji wa Matumizi
Endelevu ya Maeneo ya Maji kinachofanyika mjini Morogoro leo Januari 26, 2026.
Washiriki
wakiwa katika Kikao cha Maandalizi ya Mpango kazi wa Kitaifa na hatua za utekelezaji
wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji kinachofanyika mjini Morogoro leo
Januari 26, 2026.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Finahappy Kimambo alisema mwananchi wa kawaida anaweza kunufaika na mpango kazi huo kwa kupitia shughuli anazofanya zikiwemo uvuvi na kilimo cha mwani.
Aliongeza kuwa Serikali
imeamua kuandaa mpango kazi wa matumizi endelevu ya maji kwasababu kwenye
bahari kama ilivyo nchi kavu kuna shughuli na wadau wakiwemo wavuvi,
wasafirishaji, wachimbaji wa madini na mafuta hivyo, ili kuwa na matumizi
endelevu lazima kuwe na mpango wa matumizi.
Kikosi kazi cha
kuandaa Mpango kazi wa Matumizi Endelevu ya Maji na utekelezaji wake kinaundwa
na wataalamu kutoka Wizara za kisekta, taasisi za serikali na wadau wa
maendeleo.
0 Comments