Yanga SC imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (#CAFCL) uliochezwa leo January 31,2016 kwenye Uwanja wa New Aman kisiwani Zanzibar.
Katika mchezo huo, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao, lililofungwa na beki wake wa kati, Ibrahim Bacca, huku Al Ahly wakisawazisha kipindi Cha Pili kupitia Kiungo wao wa kati na raia wa Mali,Ally Dieng kwa Mpira wa Kona uliokufa hivyo timu hizo kugawana pointi moja.
Sare hiyo inaacha Yanga na pointi Tano (5) nafasi ya Pili , huku Al Ahly wakiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wakiwa na Point Nane (8).

































0 Comments