6/recent/ticker-posts

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali aitaka SUZA kuonesha mfano utoaji wa huduma kwa jamii



Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshmiwa Khadija Salum Ali, amewataka Watendaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuwa watendaji katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Aliyasema hayo leo 30, Januari 2026 katika Kikao kazi cha wawajibikaji wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Chuo hicho, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Ameeleza kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa kufata kanuni, sharia na ilani ya nchi ili waweze kutoa huduma zenye viwango.
Aliendelea kwa kutoa shukrani kwa watendaji wa Chuo kikuu kwa juhudi zao na kuwataka waendelee kuwa na moyo wa uvumilivu, upendo na mshikamano katika kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa jamii.
Vilevile aliwapongeza watendaji hao kwa ubunifu walioufanya kwa kuanzisha Program mbalimbali na kuhakikisha wanaongeza pato la taifa
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar Profesa Abdutalib Abdallah ameeleza kuwa chuo kimejipanga katika kuanzisha program mpya za masomo zinazoendana na ajira. Na kuanzisha majarida ya kitaalamu ya sayansi na Kiswahili.
Ameongeza kuwa chuo kimepanga kuanzisha kituo cha afya kwa ajili ya matibabu ya meno ili kiweze kutumika kwa wanafunzi wa kada hiyo
Nae Mtendaji wa Chuo hicho Dokt Meri ameomba chuo kiweze kutengeneza namna ya kuwashajihisha wanawake katika kujiunga na chuo ili waweze kupata fursa.


 

Post a Comment

0 Comments