6/recent/ticker-posts

Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Jakaya Kikwete Azindua Jengo la Ofisi na Makaazi ya Askari Pemba

Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wapili kulia) akipiga makofi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene(wapili kushoto),Kamishna Jenerali wa Uhamiaji.Dkt.Anna Makakala(wakwanza kulia) na wakwanza kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan, wakati wa  Uzinduzi wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji na Makazi ya Askari,wilayani Micheweni,mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni  sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Tatu Burhani kabla ya uzinduzi  wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji na Makazi ya Askari,wilaya ya Micheweni,mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni  sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene na wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


 

Post a Comment

0 Comments