6/recent/ticker-posts

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Hemed Suleiman Amefungua Barabara ya Finya Mkoa wa Kaskazini Pemba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikata utepe kuzindua Barabara ya Finya Kicha kwa niaba ya barabara za Mapofu Tumbe Kojifa hadi Bandarini zenye urefu wa Kilomita 21.1 Ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 62 ya  Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema ujenzi wa Barabara utarahisisha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa kuweza kuzifikika kwa urahisi zaidi. 

Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Finya kicha kwa niaba ya barabara ya Mapofu -Tumbe Kojifa hadi bandarini ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Amesema miundombinu ya barabara ni muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yoyote ile dunia hivyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujenga barabara kwa kiwango cha lami ili kurahisisha huduma ya usafiri na usafirishaji mijini na Vijijini. 

Mhe. Hemed amesema Serikali  imeshaiagiza Wizara ya Ujenzi na uchukuzi kusimamia suala la ulipaji fidia wananchi ambao nyumba zao ziliathirika kutokana na ujenzi wa barabara hio na kuwataka wananchi ambao bado hawajalipwa kuendelea kuwa na subra wakati Serikali ikiendelea na utaratibu wa malipo ya fedha zao. 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewakumbusha wananchi wa Kaskazini Pemba hususan madereva kuzitumia kwa umakini baraba hizo kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha majanga na ajali  zisizo za lazima zinazoendelea kugharimu maisha ya watu na mali zao. 

Mhe. Hemed amewata wananchi kuitunza miundombinu ya barabara na kutokujenga katika hifadhi ya barabara ili kuepuka usunbufu wakati wa ujenzi wa barabara hizo hasa zile za vijijini. 

Aidha, Mhe. Hemed ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuzisimamia vyema barabara hizo katika suala la usafi na kutoruhusu ujenzi wa vibanda pembezoni mwa barabara ili ziweze kudumu na kutumiaka muda mrefu. 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Dkt Khalid Salum Muhammed amesema kufuatia Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na kupitia awamu zote za uongozi Baraza zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami zenye kukidhi mahitaji ya watumiaji wa Baraza hizo. 

Dkt.Khalid amefahamisha kuwa katika Serikali ya Awamu ya nane (8) barabara Kilimota elf moja na themanini na nne ( 1084 ) zinaendelea kujengwa mijini na vijijini Unguja na Pemba ambapo kwa upande wa Kaskazi Pemba barabara zote zinazojengwa Mkoani humo zipo katika hatua za mwisho kumalizika. 

Amewataka wananchi wa Zanzibar kuangalia kwa umakini maeneo ya hifadhi ya barabara kabla ya kuanza ujenzi wa makaazi yao pamoja na  kuacha mafasi ya mita 30 kutoka mwanzo wa barabara ili kukwepa usumbufu wakati wa ujenzi wa miundombinu ya barabara. 

Akisoma taarifa ya kitaalamu juu ya ujenzi wa barabara ya Finya kichaka tummbe hadi Bandarini, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na uchukuzi Muhandisi Ali Said Bakari amesema ujenzi wa Barabara hizo umegharimu fedha za Kitanzania Bilioni 31.3 ambao umejumuisha daraja la michepuo liloundwa na madaraja madogo madogo 65 , njia za watembea kwa miguu na alama zote muhimu za barabarani ujenzi ambao utakwenda kuondosha changamoto ya sekta ya usafiri na usafirishaji kwa wakaazi wa maeneo hayo. 

Mhandisi Ali amewataka wakandarasi wanaondelea kujenga barabara mbali mbali Unguja na Pemba kuongeza  uharaka wa ujenzi wa miundombinu hio ili iweze kumalizika kwa haraka na wananchi waweze kufaidika na matunda ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 05 / 01 / 2026

Post a Comment

0 Comments