Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akikabidhi kitabu kinachozungumzia masuala ya mazingira kwa Katibu wa taasisi ya Green Samia Foundation Bi. Sarah Pima mara baada ya kufanya mazungumzo walipokutana jijini Dar-es-Salaam Januari 23,2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amewasihi vijana kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye masuala yanayohusiana na Muungano pamoja na Uhifadhi na Utunzaji wa mazingira ili kuleta maendeleo endelevu ya taifa.
Ameyazungumza hayo alipokutana na Taasisi ya Green Samia Foundation, jijini Dar-es-salaam Januari 23, 2026 ambao wengi wao ni vijana wanaojihusisha na Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira na kueleza kuwa wanayonafasi kubwa ya kuchangamkia fursa zinazopatikana.
Amesema kua vijana wana nafasi kubwa ya kunufaika na fursa hizo kwa kushiriki katika masuala ya mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuanzisha shughuli za kiuchumi zinazolinda mazingira kama vile biashara ya kaboni.
Amesisitiza “Muungano una unaleta umoja na ushirikiano kwa vijana, pamoja na kubuni na kutekeleza miradi ya kimazingira yenye manufaa kwa wananchi, ushiriki wao ni nguzo muhimu katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu”.
Naye Katibu wa taasisi ya Green Samia Foundation Bi. Sarah Pima ameahidi kutoa ushirikiano katika shughuli na majukumu yote ya serikali yanayo husisha uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
vilevile ameomba msaada wa kitaalamu kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (upande wa mazingira) kwa ajili ya kutoa elimu kwa vijana kuhusu utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
Dkt. Muyungi ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kuendelea kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo, rasilimali na na majukwaa ya ushiriki, ili kuongeza mchango wao katika uhifadhi wa mazingira kupitia masuala ya Muungano.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka taasisi ya Green Samia Foundation mara baada ya mazungumzo yenye kuleta tija kuhusu uhifadhi wa mazingira jijini Dar-es-Salaam Januari 23,2026.
Na.Ofisi ya Makamu wa Rais.
.jpg)
.jpg)

.jpeg)
0 Comments