Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Dkt. Richard Muyungi (katikati) akimpatia zawadi ya nakala ya kitabu
alichokiandika kinachohusu masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Bi. Maryam Juma Abdalla
wakati wa ziara yake aliyoifanya katika ofisi hiyo Januari 22, 2026 iliyolenga
kujitambulisha na kuimarisha mashirikiano baina yao. Anayeshuhudia ni
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Bi. Farhat
Mbarouk.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar zimejipanga kuhakikisha zinanufaika vyema na fursa za programu za
miradi na mikataba ya kimataifa kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Rai hiyo imetolewa Januari 22,
2026 Mjini Zanzibar na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu (Muungano na Mazingira) Dkt.
Richard Muyungi wakati wa ziara yake aliyoifanya kwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Dkt. Muyungi amesema masuala ya
mazingira na mabadiliko ya tabiachi yamekuwa na fursa kubwa duniani kwa sasa na
kwa kutambua umuhimu na uliopo Tanzania imejipanga kikamilifu kuhakikisha fursa
hizo zinawanufaisha Watanzania.
Akitolea mfano amesema kwa sasa biashara
ya kaboni duniani inazalisha kiasi cha dola trilioni 1.3 pesa na hivyo kuwa ni
mojawapo ya biashara muhimu ya kiuchumi kwa mataifa mbalimbali ambayo Tanzania pia
imeipa msukumo wa kutosha katika kuinufaisha jamii.
“Biashara ya kaboni kwa sasa ni
fursa adhimu kwa sasa duniani, jambo kubwa lenye umuhimu ni kuhakikisha
tunawajengea uwezo Wataalamu wetu badala ya kutumia washauri elekezi na hii
itasaidia kubaini kiwango halisi cha kaboni na faida za kifedha zinazoweza kupatikana”
amesema Dkt. Muyungi.
Amesema katika kuhakikisha
biashara ya kaboni italeta manufaa makubwa kwa Watanzania, Serikali tayari imekijengea
uwezo Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) sambamba na kujenga uwezo kwa wataalaam waliopo.
“NCMC kwa sasa ipo rasmi na
tayari menejimenti yake imekabidhiwa vitendea kazi muhimu ikiwemo magari ili
kuanza shughuli zake katika kubaini na kuanisha fursa za biashara ya kaboni na
kutoa elimu kwa wananchi” amesema Dkt. Muyungi.
Aidha Dkt. Muyungi amesema Ofisi
ya Makamu wa Rais itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar kufanikisha upatikanaji wa fedha na uandishi wa maandiko ya miradi ya
mazingira na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Amesema katika bara la Afrika kwa
sasa, Zanzibar imekuwa nchi ya kwanza inayoongoza katika uzalishaji wa zao la
mwani ambalo linatokana na mazao ya bahari, na hivyo Serikali zote mbili
zitahakikisha zinaweka mkazo wa kutosha katika upatikanaji rasilimali fedha za
usimamizi wa miradi.
“Tuna mikataba mbalimbali ya
masuala ya mazingira ikiwemo Basel, Nairobi na mingineyo ambayo ni vyema sasa kuhakikisha
Watalaamu wetu wanaangalia namna bora ya kuhakikisha rasilimali za bahari
zinawanufaisha wananchi” amesema Dkt. Muyungi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Bi. Maryam Juma Abdalla amemshukuru Dkt.
Muyungi kwa ziara hiyo ya kikazi na kuongeza kuwa Ofisi yake ipo tayari kuimairisha
mashirikiano yaliyopo kwa manufaa ya Serikali zote mbili.
Akizungumzia miradi ya mazingira,
Bi. Maryam amemuomba Dkt. Muyungi kuziomba taasisi za kimataifa kuipata fedha za
kutosha na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kuweza kutekeleza miradi ya mabadilkiko
ya tabianchi ambayo kwa sasa yameanza kuleta athari mbalimbali.
“Hapa Zanzibar hususani maeneo ya
Pemba kuna athari za wazi za mabadiliko ya tabianchi ambazo zinazidi kuongezeka
ikiwemo kina cha bahari na kuingia kwa maji ya bahari katika makazi ya wananchi”
amesema Bi. Maryam. .jpg)
Watendaji Waandamizi wa Ofisi ya Makamu
wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar wakifuatilia kikao baina
ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Maryam Juma Abdalla na Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi Januari 22, 2026 iliyolenga kujitambulisha
kwake na kuimarisha mashirikiano baina yao..jpg)
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
akionesha nakala ya kitabu alichokiandika kinachozungumzia masuala ya mazingira
na mabadiliko ya tabianchi kwa Viongozi na Watendajiw a Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar na Watendajiw a Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kikao
baina ya Ofisi hizo Januari 22, 2026 kilicholenga kujitambulisha kwake na kuimarisha
mashirikiano baina yao.
Watendaji Waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar wakifuatilia kikao baina ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Maryam Juma Abdalla na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi Januari 22, 2026 iliyolenga kujitambulisha kwake na kuimarisha mashirikiano baina yao.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
.jpg)
0 Comments