Kamishna Mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Ofisi ya Zanzibar, Mhe. Khatibu Mwinyi Mwinyichande, amewanasihi watumishi wa Tume hiyo kuendelea kuwatii viongozi wao na kujituma katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kamishna Mwinyichande, ametoa nasaha hizo, wakati akiwaaga watumishi wa THBUB ofisi za Pemba na Zanzibar kufuatia kustafu katika utumishi wake katika Tume hiyo.
Amewasisitiza watumishi hao kuendelea kujifunza zaidi na kukubali kukosolewa pale wanakapokosea ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika hafla hiyo, kwa niaba wa wafanyakazi wa ofisi hizo, Naibu Katibu Mtendaji THBUB, Bw. Juma Msafiri Karibona amemshuru Kamishna Mwinyichande kwa ushirikiano alioutoa wakati wote alipotumikia Tume hiyo pamoja na kusifu busara, uadilifu na hekma alizozionesha kwa watumishi wa Tume hiyo.
Jumla ya Makamishna sita wa THBUB walistaafu nyadhifa zao baada ya kuitumikia Tume hiyo, Januari 16, 2026, akiwemo Mwenyekiti Jaji Mst. Mhe. Mathew P.M. Mwaimu, Makamu Mwenyekiti Mhe. Muhammed Khamis Hamad.
Makamishna wengine waliostaafu THBUB ni Kamishna Amina Talib Ali, Kamishna Nyanda Shuli na Kamishna Thomas Masanja.
.jpg)
0 Comments