6/recent/ticker-posts

HUDUMA BORA NA UADILIFU NI MSINGI WA KUJENGA IMANI KATI YA JESHI LA POLISI NA JAMII


Na Issa Mwadangala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Wilaya ya Mbozi kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu, huku wakihakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Wito huo ulitolewa Januari 21, 2026, wakati Kamanda Senga alipokuwa akizungumza na askari hao mara baada ya kufanya ukaguzi rasmi Wilayani humo, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Polisi Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe, ukiwa na lengo la kuboresha utendaji wa kazi pamoja na kuendelea kujenga taswira chanya ya Jeshi la Polisi katika jamii.

Vilevile, Kamanda Senga alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa nidhamu, kutenda haki, kuzingatia weledi na uadilifu, sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi, huku akieleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na jamii, hali itakayosaidia kupatikana kwa taarifa fiche na hatimaye kutokomeza vitendo vya uhalifu ndani ya Wilaya hiyo.

Mwisho, Kamanda Senga aliwataka askari hao kuchukia na kupambana na rushwa kwa vitendo, huku wakihakikisha wanachukua hatua kali dhidi ya vitendo hivyo, pia aliwahimiza kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Wilayani humo ili kujiongezea vipato halali na kuishi maisha yenye heshima ndani na nje ya utumishi wao.



 

Post a Comment

0 Comments