Na Ali Abass
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mipango,Fedha na Utawala,Prof. Salum Seif Salum amewahimiza waratibu wasimamizi wa vikao wa SUZA, kuleta mabadiliko yatakayo saidia kukuimarisho Chuo hicho.
Amezuzungumza hayo wakati akimuakilisha Kaimu Makaomu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Abdi Talib Abdalla katika ofisi za Makao Makuu SUZA , Tunguu wakati alipofunga Mafunzo ya siku Nne (4) waratibu hao, ya kuzingatia itifaki,uendeshaji wa vikao, uchukuaji wa kumbukumbu za mikutano,kukaribisha wageni na kuwahudumia na kanuni za kuendesha vikao.
Prof. Salum aliwataka waratibu hao kuzingatia mafunzo waliopewa, kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya kisheria kama walivyoelekezwa katika mafunzo hayo pamoja na kuwa mabalozi wazuri kwa wafanyakazi wenzao.
Aidha alitumia fursa hiyo kutoashukurani zake kwa muendesha mafunzo ,Bwn Josephat Buhenyenge,kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,na kumuahidi kuwa SUZA itayafanyia kazi mafunzo yote aliyoyatoa.
Kwa upande wake muendesha mafunzo hayo ambae pia ni Afisa Mwandamizi Utawala kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Bw. Josephat Buhenyenge, alitoa shukurani zake kwa SUZA, na kuahidi kwamba wakati wote atakua bega kwa bega na kuunga mkono harakati zote maendelo zitakazofanyika ndani ya chuo hicho.
Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamesaidia kuonesha bengo lililopo na yatasaidia kuziba bengo hilo.
Mafunzo hayo ya siku Nne yalianza tangu Januari 21,2026 na kutamatika Januari 24,2026.

0 Comments