6/recent/ticker-posts

Balozi Seif akabidhi Kompyuta kwa Walimu Skuli ya Balozi Seif Ali Iddi Bumbwini





Makamo wa pili mstaafu wa Awamu ya Saba Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali Pamoja na Wizara kwa nguvu na juhudi kubwa wanazozionesha katika Sekta ya Elimu.

Aliyasema hayo leo tarehe 14 Febuari 2026 wakati akikabidhi Kompyuta kwa Walimu katika Ukumbi wa Skuli ya Balozi Seif Ali Iddi huko Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Serikali imejitahidi kuboresha Miundombinu katika Sekta ya Elimu, lengo ni kuona Wanafunzi wanafanya vizuri katika matokeo yao ili kutengeneza viongozi bora wa baadae.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshmiwa Lela Muhammed Mussa amesema, kupatiwa vifaa hivyo walimu hao itawarahisishia utekeleaji wa majukumu yao hasa katika wakati huu wa sayansi na teknolojia.
Aidha amesema Wanafunzi wanadeni kubwa la kulipa kwa mlezi wao, hivyo hawanabudi kufanya vizuri katika masomo yao na kuleta matokeo yatakayompa ari na nguvu ya kendelea kuwasaidia.
Mbunge Jimbo la Bumbwini Mheshmiwa Mwinyi Jamal Ramadhan amemshkuru balozi seif kwa jitihada nzuri aloifanya kwani ameonesha azma, dhamira na kujitoa katika kuisaidia sekta ya elimu.
Nao walimmu waliopatiwa vifaa hivyo wamemshkuru Balozi Seif na wameahidi wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.
Imetolewa na kitengo cha habari Mawasiliano na Uhusiano (WEMA)

 

Post a Comment

0 Comments