Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akiwa
ameambatana na Kamishna wa Fedha na Lojistiki CP
Liberatus Sabas pamoja na maafisa wengine amefanya
ukaguzi wa maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba za Wakufunzi na Familia zao na Mabweni ya Wanafunzi katika shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Ujenzi huo unatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya majenzi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Jeshi la Polisi.
Itakapo kamilika miradi hiyo katika Shule hiyo ya Polisi Moshi utawaongezea morali katika utendaji kazi sambamba na kukuza ustawi wa askari kwa kukaa na kuishi kwenye mazingira bora na ya kisasa jambo litakalo wawezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mbali na uboreshaji huo wa miundombinu ya makazi ya
wakufunzi na wanafunzi upo uboreshaji wa mitaala ambao
umefanyika sambamba na kuingia kwenye mikataba na vyuo
vya ndani ya nchi ili kuendana na utekelezaji wa
Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai iliyopendekeza Askari
kujengewa uwezo ambapo imewezesha Maafisa, Wakaguzi na
Askari 111 kufanikiwa kuhitimu masomo katika kiwango cha
Uzamili (Masters) kwa mwaka 2025 kutokana na uwepo wa
Tawi la IAA (Institute of Accountancy Arusha) katika Shule
hiyo ya Polisi Moshi ambao wanaendesha kozi mbalimbali za
kuwajengea uwezo na ujuzi Askari kwa kushirikiana na Jeshi
.jpg)

.jpg)
%20(1).jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments