6/recent/ticker-posts

Kamati ya Sheria na Utawala ya Baraza la Jiji Zanzibar yabadilishana uzoefu na Manispaa Magharibi ‘A’ (Kianga)



Kamati ya Sheria na Utawala ya Baraza la Jiji Zanzibar imefanya ziara ya kikazi katika Manispaa Magharibi ‘A’ (Kianga), kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya kisheria, kiutawala na usimamizi wa huduma za jamii.
Ziara ilianza kwa kikao cha pamoja ambapo wajumbe walijadili uendeshaji wa kamati za sheria, ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miundombinu. Walisisitiza kuimarisha ushirikiano ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.
Wajumbe walitembelea Kituo cha Gari za Abiria Mndo, wakajionea mafanikio na changamoto (k.m. upangaji wa maegesho na udhibiti wa usafirishaji), na kuahidi kutoa ushauri kwa mamlaka husika.
Pia walizuru Soko la Chuini na kuangalia usafi wa mazingira, hasa mitaro ya maji taka. Walipongeza jitihada za Manispaa na kusisitiza ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuzuia magonjwa.
Ziara ilihitimishwa kwa kutembelea Diko la Ngalawa, ambapo walipokea maelezo kuhusu miundombinu na changamoto. Kamati iliridhika na jitihada za Manispaa Magharibi ‘A’ na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa manufaa ya wananchi.
(Na Maua Abdulla, BMMA)


 

Post a Comment

0 Comments