6/recent/ticker-posts

KIST wakutana na wadau wa Uhandisi Ujenzi na maji safi na maji taka



 Uongozi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) umekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa Uhandisi Ujenzi na maji safi na maji taka.

lengo la mazungumzo hayo ni kuweka mashirikiano katika suala zima la Kitaaluma pamoja na uanzishwaji wa Mafunzo na kutoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa maendeleo ya sekta ya ujenzi Zanzibar.
Ujumbe huo uliongozwa na Bwana Ravindra Gettu ambae ni Profesa katika Taasisi ya Indian Institute of Technology Madras (IITM) akiambata na Ujumbe wake.
Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa Taasisi umeridhishwa na ujio wa wadau hao muhimu na kuwahakikishia kuwa Taasisi ipo tayari kushirikiana nao katika kufanikisha utoaji wa Mafunzo pamoja na kutoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa Taasisi ya Karume.

Post a Comment

0 Comments