Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Zanzibar , Dkt. Aboud Suleiman Jumbe , akiwa ameambatana na Maafisa mbali mbali wa Serikali na Shirika la Bandari Zanzibar, Idara ya Uhamiaji Tanzania na Maafisa wengine wakiwa katika ziara na Mapokezi maalum ndani ya Meli ya Crystal Symphony iliyotia nanga katika Tishali la Abiria Malindi. Zanzibar .
Meli hii aina ya Crystal Symphony inayoongozwa na Nahodha wake (Cpt) Tonci Hladilo ina Urefu wa Mita 238.01m na Uzito (GRT) 51,068t ikiwa na Idadi ya Abiria 606 na Mabaharia 488 .Hizi zote ni Sehemu ya Jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.@samia_suluhu_hassan na Rais wa Zanzibar na Menyekiti wa baraza la Mapinduzi @dr.hmwinyi walizofanya kutangaza Vivutio vya Utalii ndani na nje ya Tanzania
Akizungumza mara baada ya ziara fupi ndani ya Meli hiyo Dkt. Jumbe ameeleza kuwa ni moja ya Meli kubwa zaidi za kitalii zinazofanya ziara duniani kote, na kuwasili kwake katika bandari ya Zanzibar kunatoa nafasi kubwa ya kukuza Utalii na Uchumi wa Zanzibar kutokana na Uwezo wa kutoa huduma za kifahari za kiwango cha juu.
Ujio wa Meli hii Unachochea na Kwenda Sambamba na Mikakati Imara ndani ya Siku 100 za Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipoapishwa na kuingia Madarakani kwa awamu ya Pili ya Urais .
Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kuwa na Mikakati ya kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii kama moja ya sekta muhimu kwa Uchumi wa Zanzibar. hivyo, tukio la kupokea meli hii linadhihirisha juhudi za Serikali katika kuongeza Vivutio vya Kitalii, kuboresha huduma za Utalii, na kuleta Maendeleo Endelevu kwa wananchi wa Zanzibar.
Katika hotuba yake, Dkt. Jumbe alielezea furaha yake kwa kuweza kufanya ziara fupi ndani ya Meli hii na kusema kwamba ni ishara nzuri ya kuendelea kwa maendeleo ya Utalii katika kisiwa cha Zanzibar.
Aidha Kupokea Meli kubwa ya Kitalii aina ya Crystal ni hatua kubwa kwa Zanzibar katika kukuza Sekta ya Utalii na kuimarisha Uchumi wake. Ni Uthibitisho wa Juhudi zinazofanywa na Serikali ya Dkt. Mwinyi katika kuendeleza Sekta hii Muhimu. Tunatarajia kuwa hatua hizi zitasaidia kujenga Zanzibar kuwa moja ya Maeneo ya kivutio bora cha Utalii cha kimataifa



0 Comments