Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd, Abdalla M. Mussa ametembelea Ofisi ya Naibu Waziri wa Elimu Na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Khadija Salum Ali kwa ajili ya mazungumzo ya kujenga Taasisi pamoja na maendeleo yanayofanywa na Taasisi ya Elimu katika kuendelea kuutangaza Mtaala na kuboresha utendaji kazi.
Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi alisisitiza dhamira ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha mtaala mpya unafahamika kwa jamii na walimu, sambamba na juhudi za kuboresha utendaji kazi kupitia programu za mafunzo na mikakati ya kitaaluma.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano (TEZ)


0 Comments