6/recent/ticker-posts

Naibu Waziri Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji afanya ziara Vituo vya kupigia Kura katika Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar



Naibu Waziri Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Mhe Hassan Khamis Hafidh amesema kukamilika kwa Uchaguzi wa Baraza la Vijana kwa ngazi ya Shehia kutasaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji kupanga mikakati madhubuti ya kuwasaidia Vijana kiuwezeshaji na kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana wa Zanzibar
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Vituo vya kupigia Kura katika Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar kwa ngazi ya Shehia kwa Wilaya zote za Pemba amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Vijana wote wa Zanzibar wanakuwa na shighuli za kufanya itakahayomuingizia kipato chake na Taifa
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua uwepo wa changamoto ya ajira na uwezeshwaji kwa Vijana wa Zanzibar ndio ikaanzisha Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
"Niwaambie Vijana Wizara yenu hii itahakikisha inatafuta fursa za ajira ndani na nje ya nchi ili Vijana waweze kuajiriwa katika sekta binafsi, Serikali na kujiajiri " alisema Naibu Waziri huyo
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Khalid Masoud Waziri amesema Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar ni fursa ya kipekee kwa Vijana kuchagua Viongozi watakaoweza kuwasemea changamoto zao na kuwaletea maendeleo Vijana kuanzia ngazi za Shehia hadi Taifa
Aidha ametumia fursa hiyo kuwapongeza Vijana wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya Shehia na Wilaya hali ilionesha ukomavu wa demokrasia na kuonyesha uwezo wao wa kuongoza kwa ufanisi mkubwa
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar amesema Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar kwa ngazi ya Shehia umeendeshwa na kukamilika kwa asimilia kubwa na kwa Shehia zote za Unguja na Pemba
Aidha amewaomba Vijana wote ambao kura zao hazikutosha kuyokuvunjika na kuendelea kutoa mashirikiano kwa Viongozi ili kusaidia upatikanaji wa fursa za maendeleo ya Vijana katika Shehia zao
Aidha amewasisitiza Vijana umuhimu mkubwa wa kujitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii jambo ambalo litasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.


 

Post a Comment

0 Comments